Thursday 5 March 2015

Ronaldo ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani

*Aendelea kumtesa Lionel Messi

 
LONDON, England
CRISTIANO Ronaldo (pichani) ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani huku akiwa na utajiri wa kiasi cha pauni Milioni 152 ikiwa ni pauni 7 zaidi ya mpinzani wake Lionel Messi.

Baada ya kufanya vizuri mwaka 2014 na kushuhudia Ronaldo akiiwezesha Real Madrid kupata mafanikio katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kushinda tuzo ya Ballon d'Or, aliongeza tofauti ya nafasi ya utajiri wake na nyota huyo wa Barcelona na Argentina.

Kwa mujibu wa orodha ya matajiri iliyotolewa na Goal.com Alhamisi, Ronaldo na Messi ndio wanaotamba kwa utajiri zaidi kuliko wanasoka wengine kwa sasa katika soka la kulipwa.
Jumla ya utajiri wao, ambao unatokana na matangazo pamoja na mishahara na bonasi, ni zaidi ya ule alionao Neymar, anayeshika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa thamani ya pauni Milioni 97.9.

Zlatan Ibrahimovic wa Paris Saint-Germain na Sweden anautajiri wa Pauni Milioni 76.1, wakati Wayne Rooney wa Manchester United ndiye anayeongoza kwa utajiri kwa wachezaji Waingereza akishika nafasi ya tano kwa dola Milioni 74.6.

Kaka wa Brazil yeye kwa sasa anashikilia nafasi ya sita akiwa na pauni Milioni 69.6, akifuatia na Samuel Eto'o (pauni Milioni 63.1), Raul (pauni Milioni 61.6) na  Ronaldinho (Milioni 60.2).

Kiungo wazamani wa England Frank Lampard, kwa sasa anaichezea Manchester City kabla yakwenda New York City katika Ligi Kuu ya Marekani, anakamilisha orodha ya 10 bora kwa kuwa nba utajiri wenye thamani ya pauni milioni 58.

Wachezaji wengine Waingereza waliopo katika 20 bora ni Rio Ferdinand (nafasi ya 12, pauni Milioni 52.2), Steven Gerrard (nafasi ya 14, pauni Milioni 46.4) na John Terry (nafasi ya 20, pauni Milioni 40.6).

Lionel Messi wa Barcelona.
Kuna wachezaji wengine wawili zaidi wa Man City katika orodha hiyo, pamoja na Yaya Toure katika nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa pauni Milioni 44.9 na Sergio Aguero katika nafasi ya 19 na utajiri wa pauni Milioni 42.

Mwaka jana orodha ya matajiri wa Goal iliyotolewa ilibainisha kuwa Ronaldo alikuwa na utajiri wenye thamani ya pauni Milioni 122, huku Messi akimkimfuatia kwa nyuma kwa utajiri wa pauni Milioni 120.5.

No comments:

Post a Comment