Sunday, 1 March 2015

Mwili wa Kapteni Komba kuagwa Karimjee leo


Kapteni John Damiani Komba.

Na Mwandishi Wetu
MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa kundi la The Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba aliyefariki Jumamosi jioni, unatarajia kuagwa leo Jumatatu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach eneo la Tangi Bovu, baada ya kuagwa mwili huo Jumanne utasafirishwa kwa ndege kwenda Mbinga kwa mazishi.
Aidha, Jumapili viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi na serikali akiwemo Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete walifika nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa wafiwa akiwemo mke wa marehemu Salome.
Mbali na Kikwete wengine waliofika nyumbani hapo kwa marehemu ni pamoja na mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chandema) Dr. Wilbroad Slaa, Abdulhaman Kinana na wengineo wengi.
Komba alifariki Jumamosi njiani akikimbizwa katika hospitali ya TMJ Mikocheni, baada ya kuzidiwa na kisukari na shinikizo la damu akiwa nyumbani kwake Mbezi Beachi eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mipango wa TOT Gasper Tumaini alithibitisha kifo cha Komba Jumamosi na kusema kuwa mipango inaendelea nyumbani kwake.
Bwana Alitoa na Bwana alitwaa jina lake lihimidiwe, Amina.

No comments:

Post a Comment