Thursday 31 May 2018

Nuru Kombo Kidedea Filbert Bayi School Bonanza

Mkurugenzi wa Shule za fFlbert Bayi, Anna Bayi akiwakabidhi kikombe washindi wa jumla bonanza la 11 la Shule za Filbert Bayi (iIterhouses), wachezaji wa timu ya Red House,   Benson Peter (katikati) na Johari Onguye.
Mwanariadha Nuru Kombo ameibuka kidedea kwa kutwaa medali mbili za dhahabu kwenye mbio za mita 100 na 200 katika mashindano ya Filbert Bayi Schools Inter Houses Sports Bonanza.
 Mashindano hayo ya siku mbili yalianza Juzi Jumatano kwenye viwanja vya Filbert Bayi Kibaha Mkuza mkoani Pwani.

 Katika mbio za mita 100, Nuru alikimbia kwa sekunde 16:13 na kuwapiku Shyrose Christopher aliyemaliza wa pili akikimbia kwa sekunde 17:03 na Khadija Issa aliyekimbia kwa sekunde 18:59.

 Kwenye mbio za mita 200, Nuru tena alitwaa dhahabu akikimbia kwa sekunde 36:24 na kuwapiku Shyrose aliyemaliza wa pili akikimbia kwa sekunde 36:91 na Khadija aliyemaliza wa tatu akikimbia kwa sekunde 37:29.

 "Napenda riadha, nimekuwa nikijifua mara kwa mara na nina ndoto ya kuja kuwa msomi na mwanariadha nyota wa kimataifa  baadae," alisema Nuru ambaye ni mwanafunzi wa sekondari wa Shule ya Filbert Bayi.
 
Katika mbio za mita 400, Hidaya Jongo aliibuka kidedea akikimbia kwa dakika 1:20:86 huku Salome Edger akimaliza kwenye nafasi ya pili baada ya kukimbia kwa 1:22:31 na Nuru akaambulia medali ya tatu akikimbia kwa dakika 1:27:01.

Upande wa wavulana, Benson Mlacha aliibuka kinara akikimbia kwa dakika 1:03:97 huku Twalibu Abdallah aliyekimbia kwa dakika 1:04:21 na Amos Leonard aliyekimbia kwa dakika 1:04:56 wakitwaa medali ya fedha na shaba.

Kwenye mbio za mita 200, Abdallah Fauz aliibuka kinara akikimbia kwa sekunde 28:81 na kuwapiku Valentino Peter aliyekimbia kwa sekunde 29:63 na Henry Sebastian aliyekimbia kwa sekunde 29:82 na kumaliza kwenye nafasi ya pili na tatu.

Kwenye mbio za mita 100, Stanley Benson aliibuka kidedea akikimbia kwa sekunde 11:89 na Faris Jaffu alimaliza wa pili akikimbia kwa sekunde 12:01 na Clement Mgaya alihitimisha tatu bora akitumia sekunde 14:22 kumaliza mbio.

Mwenyekiti wa FBF, Filbert Bayi alisema katika mashindano hayo ya siku mbili wanafunzi wa shule hizo walichuana kwenye soka, netiboli na riadha.


"Michezo ni sehemu ya ukuaji mzuri kwa watoto, pia inawaongezea uelewa mzuri, hivyo shule zetu zimekuwa na siku maalumu ya michezo kila mwaka," alisema Bayi ambaye anashikilia rekodi ya Jumuiya ya Madola ya mbio za meta 1500, ambayo haijavunjwa kwa miaka 44 sasa.

NB:Matokeo ya Jumla ya bonanza hilo yatafuata baadae.

TAA, KOICA WASAINI MAKUBALIANO YA MAFUNZO

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA BW, RICHARD MAYONGELA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MAKUBALIANO YA MAFUNZO  PAMOJA NA SHIRIKA LA KUTOA MISAADA UPANDE WA TANZANIA (KOICA) HUKU AKISHUHUDIWA NA MKURUGENZI MKAAZI WA KOICA BW, JOONSUNG PARK    LEO KATIKA HOTEL YA HYATT JIJINI DAR ES SALAAM.
KAIMU   MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA BW, RICHARD MAYONGELA (KUSHOTO) NA MKURUGENZI MKAAZI WA KOICA BW, JOONSUNG PARK WAKISAINI MKATABA WA MAFUNZO LEO JIJINI DAR ES SALAAM. 

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA BW, RICHARD MAYONGELA (MWENYE TAI NYEKUNDU KUSHOTO), MKURUGENZI MKAAZI WA KOICA  BW, JOONSUNG PARK (  KATIKATI) NA MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR BW, MUHIDIN TALIB ABDULLAH  WAKIONYESHA MKATABA WA MAKUBALIANO MARA BAADA YA KUWEKA SAINI KATIKA HOTEL YA HYATT  JIJINI DARE ES SALAAM MAPEMA LEO.
KUTOKA KUSHOTO NI MENEJA RASILIMALI WATU(MAFUNZO) BW, ABDI MKWIZU NA AFISA SHERIA MWANDAMIZI BI NURU NYONI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEZO JUU  YA MKATABA WA MAKUBALIANO WA MAFUNZO KATI YA  MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA NA SHIRIKA  LA KIMATAIFA LA MISAADA LA  KOREA (KOICA) MAPEMA LEO KATIKA HOTELI YA HYATT JIJINI DAR ES SALAAM.
MKURUGENZI MKAAZI WA KOICA BW, JOONSUNG PARK  AKITOA MAELEZO MAFUPI KABLA YA KUWEKA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUTOA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE  (TAA) LEO KATIKA HOTEL YA HYATT JIJINI DAR ES SALAAM. 

MultiChoiceYawekeza Kukuza Tasnia ya Filamu Afrika


Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson (katikati), Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harison Mwakyembe (Kulia) na Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.,Maharage Chande wakishuhudiauzinduzirasmi wa programu ya‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoafursakwavijanawenyekipajikatikatasniayafilamukujiunganakituomaalum cha mafunzoyafanihiyokwamuda wa mwakamzimakwaudhamini wa MultiChoiceAfrika. Uzinduzihuoulifanyikajijini Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MultiChoiceAfrica,Imezindua rasmiprogram kubwayakijamiiinayolengakuletamapinduzimakubwakatikatasniayafilamuhapa Tanzania nabaraniAfrikakwaujumla.

Program hiyoijulikanayokamaMultiChoice Talent Factory (MTF) –inalengakuchocheaubunifu wa vijana wa Afrikakatikatasniayafilamunaimeandaavyuomaalumvitatuambavyovitatoamafunzomaalumyautengenezaji wa filamukwavijanakutokanchimbalimbalikotebaraniAfrika.

“Maendeleoyanchiyetukwamudamrefuyamekuwayakitambuliwakwauwekezajikatikamaliasilinyingitulizonazokama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, nakadhalikahukusektayaubunifuikiwahaijapewakipaumbelekikubwanahivyosektayasanaanaubunifukuwanamchangomdogokatikaukuaji wa uchumiwetu.

Ili kuhakikishakuwatunasaidiananaserikalikatikamkakati wake wa kuifanyasektayaubunifunasanaakuwamojayamihimiliyauchumiwetu, MultiChoiceimeanzisha program hiinatumeanzanasektayafilamu” alisema Maharage Chande, Mkurugenzi wa MultiChoicekandayaAfrikaMasharikinaMagharibi.

Tumebarikiwakwavipajivingikatikafanimbalimbalinabilashakatukiwekezakatikavipajivyavijanawetubilashakatutafanikiwakupanuawigo wa ajiranauchumiwetunahivyokuchangiakwakiasikikubwaukuaji wa uchumi wa nchiyetu


Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda yaAfrikaMasharikinaMagharibi Maharage Chande akizungumzawakati wa uzinduzirasmi wa programuya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoafursakwavijanawenyekipajikatikatasniayafilamukujiunganakituomaalum cha mafunzoyafanihiyokwamuda wa mwakamzimakwaudhamini wa MultiChoiceAfrika. Uzinduzihuoulifanyikajijini Dodoma

AmesemaProgrammu hiyo itakayoanza rasmi mwezi Oktobamwakahuuitawawezeshavijana
wanne
kutoka Tanzania kuungananavijanawenginekutokanchimbalimbalizaAfrikakatikavyuomaalumvyamafunzoyautengenezaji wa filamambavyovitakuwanchini Nigeria, Kenya na Zambia.
Kwaupande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa naMichezo Dr. HarisonMwakyembeamesema program hiyoitakuwachachukubwakatikakuletamapinduzikwenyetasniayafilamuhapanchinikwanivijanawatakaopatikanambalinakwambawatakuwanauwezo wa haliyajuu wa kutengenezafilamu, palipiawatakuwakamawaalimu wa wezaoambaowanavipajikatikatasniahiyo.

“NimefurahisanakusikiakuwaMultiChoicewanapangakuendeleanampangohuukwamudamrefukwahiyojapokuwatunaazakwakupelekawanafunziwanne, badotunaaminihuunimwanzomzurisana. Cha msingi kwanza siyoididiyawanafunzi, baliniumuhimu wa chuohichonakiwango cha mafuzokitakachotolewa. Tunaaminikwamwakahuu wa kwanza vijanahaowakikamilishamafuzoyaonawakirudinyumbaniwatakuwachachukubwakatikakukuzanakuimarishatasniayafilamuhapanchini”
PiaametoaraikwaMultiChoicekushirikianakwakaribunawizarayaElimunaMafunzoyaUfundinapiavyouvyetuambavyovinatoaelimuyasanaayafilamuilikuhakikishakuwawanabadilishanaujuzinauzoefunapiaikiwezekanakuwanamiradiyapamojayamudamrefunamfupinahivyokuwafikiavijanawengizaidinakuwezakutimizalengokuu la kuifanyafaniyafilamukuwamojayanguzozauchumi wa nchihii.
Program hiyoinaanzarasmikwakupokeamaombiyawashirikiambayoyatapokewakwanjiayamtandao
Kwaufupi;
·      
Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda yaAfrikaMasharikinaMagharibi Maharage Chande akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la JamhuriyaMuungano wa Tanzania Dk. Tulia Acksonkatikahaflayauzinduzirasmi wa programuya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoafursakwavijanawenyekipajikatikatasniayafilamukujiunganakituomaalum cha mafunzoyafanihiyokwamuda wa mwakamzimakwaudhamini wa MultiChoiceAfrika. Uzinduzihuoulifanyikajijini Dodoma jana.

   Programu hii inamruhusu mtanzania anayekidhi vigezo kuingia kwenye mashindano ya kupata washindi wanne ambao watadhaminiwa kwa mwaka mmoja kwa mafunzo yote yahusuyo utengenezaji filamu.

·         Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya www.multichoicetalentfactory.com
·         Vilevile kutakuwa na namba maalum ambayo inapatikana kuanzia tarehe 1 June 2018.
·         Wanaotaka kushiriki wanaweza kuanza kuwasilisha maombi yao kuanzia sasa na mwisho ni tarehe 4 July 2018.

·         Hakuna gharama za kushiriki kwenye mashindano
·         Mafuzo rasmi kuanza mwezi wa Oktoba 2018, jijini Nairobi, Kenya
·         Washindi watako chaguliwa watakuwa wanne (4).

·         Gharama zote zitalipiwa na Multichoice kwa kipindi cha mwaka mmoja
Jiungenaulingo wa MTF Mitandaonikwa #multichoicetalentfactorykishafuata au jiungekwa:
·         Instagram: @multichoicetalentfactory;
·         Twitter: @MCTalentFactory
·         Facebook: @multichoiceafricatalentfactory


KwaMaelezozaidiwasilianana;
Johnson Mshana
MkuuwaMawasiliano



Wednesday 30 May 2018

Chuo Kikuu Dar, Sweden Wajadili Njia za Kufundishia

Mkurugenzi wa KTH, Institute of Technology University Management, Profesa Roman Wyss  akifafanua jambo kwenye Mkutano wa mwendelezo wa kutekeleza  njia za kufundisha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika secta ya mawasiliano kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sweden (KTH)  katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Dk Hamisi detyabura (kulia)  akifafanua jambo kwenye Mkutano wa mwendelezo wa kutekeleza  njia za kufundishia katika sekta ya Mawasiliano kwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sweden (KTH), katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

UDSM ICT Incubator (UDICTI) Acting Coordinator, Collage of ICT, Christine Mwase, explain something during the conference of ICT held in Dar es Salaam today.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Hamisi Ndetabura (kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa KTH,  Roman Wyss (katikati) na Research Engeneer, Mats Leksell (kushoto) katika Mkutano wa mwendelezo wa kutekeleza  njia za kufundisha, chuo kikuu cha Dar es Salaam katika sekta ya mawasiliano kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sweden (KTH)  DSM uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Hamisi Ndetabura (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa KTH,  Proffesor Roman Wyss katika Mkutano wa mwendelezo wa kutekeleza  njia za kufundisha, uliofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Secta ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sweden (KTH).

Friday 25 May 2018

Yanga, Azam Kufunga Pazia Ligi Kuu Usiku Taifa

Na Mwandishi Wetu
PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara litafungwa usiku wa Jumatatu ya Mei 28, mwaka huu kwa mchezo kati ya Yanga SC na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Bodi wa Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo alisema leo kwamba mchezo huo utaanza Saa 2:00 usiku.

Wambura amesema kwamba mechi nyingine zote za kufunga pazi la Ligi Kuu msimu 2017- 2018 zitachezwa kuanzia Saa 10: 00 jioni Jumatatu ya Mei 28, 2018 kwa timu zote 16 kuingia viwanjani kukamilisha raundi ya 30 na mechi 240 za msimu huu.

Wambura,  amezitaja mechi hizo ni kati ya Maji Maji ya Songea na mabingwa, Simba SC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Lipuli na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba na Tanzania Prisons dhidi ya Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

 Mechi nyingine ni kati ya Ndanda FC dhidi ya Stand United Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Mtibwa Sugar dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Njombe Mji FC dhidi ya Mwadui FC na Mbao FC dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Wakati Ligi Kuu inamalizika Jumatatu, tayari Simba SC ndiyo mabingwa wakiwa wamejikusanyia pointi 68 katika mechi 29, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 55 za mechi 29 na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC wapo nafasi ya tatu kwa pointi zao 51 za mechi 28 na leo wanacheza mechi yao ya 29 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa.

Njombe Mji FC tayari imeshuka Daraja kutokana na kuambulia pointi 22 katika mechi 29, wakati Ndanda FC yenye pointi 26 za mechi 29 na Maji Maji FC yenye pointi 24 za mechi 29 pia mojawapo itashuka pia baada ya mechi za Jumatatu.

Wakati timu mbili zitaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu Jumatatu, tayari African Lyon, KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance Schools ya Mwanza na Biashara United ya Mara zimekwishapanda kuelekea ligi ya msimu ujao, itakayokuwa na timu 20 ambayo ni ongezeko la timu nne.

Misri Wajifua kwa Kombe la Dunia Urusi 2018

CAIRO, Misri
TIMU ya taifa ya Misri itacheza dhidi ya Kuwait kesho Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa kirafiki kati ya 15 itakayochezwa na timu hiyo ya Afrika iliyofuzu kucheza Kombe la Dunia itakayofanyika kuanzia Juni 14hadi Julai 15 nchini Urusi.

Timu za taifa ya Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia zinaliwakilisha bara ya Afrika katika Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi.

MIsri watamkosa mkali wao Mohamed Salah huko Kuwait City wakati akiichezea klabu yake ya Liverpool ambayo leo inacheza dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya leo.

Nyota mwingine wa Kombe la Dunia, Sadio Mane wa Senegal, naye pia atakuwa katika jezi ya Liverpool akijaribu kuizuia Real Madrid kutwaa taji lake la nne mfululizo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Baada ya kucheza na Kuwait, kikosi hicho cha timu ya taifa ya Misri ambacho kinafundishwa na kocha wa Argentina Hector Cuper atakiongoza kwenda Ulaya kucheza na Colombia huko Milan na baadae Ubelgiji jijini Brussels.

Morocco, imerejea katika Kombe la Dunia baada ya miaka 20 ya kutokuwepo, itakwaana na timu ambazo hazijafuzu kwa Kombe la Dunia Ukraine na Slovakia katika jiji la Uswisi la Geneva kabla ya kukabiliana na Estonia huko Tallinn.

Nigeria ndio nchi pekee ya Afrika ambayo itacheza mchezo wa kujipima nguvu barani, ikiikaribisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Port Harcourt Jumatatu hii.

Timu hiyo ya 'Super Eagles' baadae itakabiliana na England kwenye Uwanja wa Wembley na Jamhuri ya Czech huko Austria kabla haijapanda ndege na kwenda Urusi, nchi ya kwanza ya Ulaya Mashariki kuandaa fainali za Kombe la Dunia.

Senegal, inashiriki kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na kutinga robo fainali, itacheza dhidi ya Luxembourg na Croatia kabla haijakutana na Korea Kusini bila wachezaji kwenye Uwanja wa Australia.

Tunisia, bila kushinda mechi 14 za Kombe la Dunia tangu ilipowafunga Mexico mwaka 1978, watakuwa ugenini wakicheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ureno kabla hawajakutana na Uturuki huko Uswisi na Hispania huko Urusi.

Nchi tani za Afrika zilizofuzu zinarejea mchezoni kwa mara ya kwanza tangu Machi wakati walipopata matokeo tofauti tofauti walipocheza mechi za kirafiki.

Misri ilichapwa 2-1 na Ureno baada ya Cristiano Ronaldo kufunga mara mbili katika muda wa majeruhi na timu hiyo iliyobadilika sana ilijikuta ikifungwa 1-0 na Ugiriki.

Morocco iliwafunga Serbia 2-1 huko Italia na kurejea nyumbani ambako walishinda 2-0 dhidi ya Uzbekistan.

Kipa Ujerumani Aendelea Kuwa Fiti Kombe la Dunia

Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer.

MUNICH, Ujerumani
KIPA wa Ujerumani Manuel Neuer yuko mbioni kuwa fiti kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia baada ya kupona maumivu ya mguu yaliyomuweka kando kwa karibu msimu mzima, alisema juzi kocha wa timu ya taifa Joachim Loew.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo katika kambi yao kaskanzini ya Italia, Loew alisema anauhakika kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni nahodha wa timu ya Ujerumani, sehemu ya timu iliyotwaa Kombela Dunia 2014, atacheza Urusi.

Neuer ambaye ni kipa wa Bayern Munich hajacheza soka tangu alipovunjika mfupa wa mguu wake Septemba mwaka jana, ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji na kumfanya kuwa katika wasiwasi wa kucheza fainali hizo.

"alifanya mazoezi wiki katika klabu ya Bayern, hapa anafanya mazoezi kamili na anaendelea kuwa fiti, “alisema Loew alipozungumza na waandishi wa habari.

"Tutaangalia mazoezi ya siku hadi siku. Ikiwa atakuwa fiti kwa asilimi 100 basi hakuna ubishi atakwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo, na kama kutakuwa na tatizo lolote, basi itabidi kuzungumza….”

Loew pia anatarajia kurejea kwa Jerome Boateng katika kikosi chake wiki hii wakati beki huyo wa kati akipona maumivu ya nyonga aliyoyapata mwezi uliopita.

"Kila kitu kinakwenda vizuri kama kilivyopangwa na wiki ijayo tunamtarajia kushirii katika mazoezi, “alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 58, ambaye mwezi huu ameongeza mkataba wake utakaompeleka hadi mwaka 2022.

Wajerumani wanajifua katika milima ya Alps nchini Italia kwa ajili ya maandalizi ya kutetea taji la Kombe la Dunia, huku Loew akiwapongeza wachezaji wake wakati wakiwa tayari kwa ajili ya kutetea taji lao.

"Hapa kuna hali nzuri sana, uwanja mzuri, hoteli nzuri sana, sehemu ya kuchezea iko katika hali nzuri sana, hivyo kila kitu kiko katika hali nzuri sana.”

Ujerumani itaaendelea kubaki Italia hadi Juni 5, siku moja baada ya siku ya mwisho ya kutangaza kikosi cha mwisho. Loew ina wachezaji 27 katika kambi hiyo huku wanne wakitarajiwa kupigwa `panga’.

Ujerumani itasafiri na kwenda kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki ugenini dhidi ya Austria huko Klagenfurt Juni 2 kabla hajarejea na kukukabliliana na Italia kabla haijarudi nyumbani kuikabili Saudi Arabia huko Leverkusen siku sita baadae, wako katika Kundi F pamoja na Sweden, Korea Kusini na Mexico.

Mashabiki England Kufurika Kombe la Dunia Urusi

Nahodha wa England, Harry Kane.

MOSCOW, Urusi
HADI mashabiki 10,000 wa soka kutoka England wanatarajia kutua nchini hapa mwezi ujao ili kuiunga mkono timu yao itakapokuwa ikicheza mechi za Kombe la Dunia mwaka huu, amesema msemaji wa Ubalozo wa Uingereza mjini hapa juzi.

Msemaji huyo akizungumza na Shirika la Habari la Urusi, Tass, alisema kuwa wanatarajia raia karibu raia 10,000 kutoka Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kwa ajili ya kuja kushuhudia fainali za Kombe la Dunia.

“Tunatarajia karibu wapenzi wa soka 10,000 kutoka Uingereza kutembelea Urusi mwaka huu kuja kushuhudia fainali za Kombe la Dunia na kuja kufurahia uhusiano mzuri kati ya Uingereza na Urusi kabla ya Kombe la Dunia kwa miaka miwili sasa.

"Ofisa wa usalama Mark Roberts (ambaye anashughulikia sera za soka) alitembelea mara mbili nchini Urusi mwaka jana, “alisema. “Msafara wa Polisi wa Uingereza walifanya kazi wakati wa mechi za Kombe la Shirikisho la Dunia kwa  Klabu Julai mwaka jana.

Gazeti la Uingereza la Daily Star wiki hii liliandika ripoti kuwa mashabiki wa soka wa England watakuwa wakitafuta kitu huko Urusi wakati wa Kombe la Dunia na hilo litakuwa kama Vita ya Tatu ya Dunia, Nne, Tano, Sita na Saba.”

Vurugu kadhaa ziliripotiwa kati ya mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Uefa huko Ufaransa kati ya Juni 10 na Julai 10, 2016. Mpambano mkubwa uliowahi kuibuka kati ya mashabiki wa Urusi na Waingereza wakati ikielekea mechi ya Juni 11 huko Marseilles.

Fainali za Kombe la Dunia 2018 zinatarajia kuanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi huku mechi ya ufunguzi ikitarajiwa kupigwa mjini hapa.

Urusi imechagua miji 11 kuchezwa fainali hizo, ambayo ni Moscow, St. Petersburg, Sochi, Kazan, Saransk, Kaliningrad, Volgograd, Rostov-on-Don, Nizhny Novgorod, Yekaterinburg na Samara.

Liverpool, Real Madrid ni Mpambano wa Kufa Mtu

Mohamed Salah wa Liverpool.

KIEV, Ukraine
HATMA mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya yanafikia tamati kesho wakati Liverpool itakapoikabiri Real Madrid katika mchezo wa fainali utakaofanyika mjini hapa.

Ulikuwa mchezo wa Kundi B kwenye Uwanja wa Bernabeu Novemba 4 mwaka 2014. Ni mfano mkubwa wa mabadiliko ya jinsi mambo yalivyobadilika kwa Liverpool wakati mambo yakiwa vile vile kwa Real Madrid.

Timu mwenyeji itakuwa na wachezaji tisa katika kikosi cha kwanza huko Kiev leo Jumamosi, wakati tofauti na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kwa upande wake.

Ni taarifa kubwa kuhusu mchezo wa makundi, ambapo Liverpool ilipoteza kwa uchache kwa bao la kipindi cha kwanza la Karim Benzema, lakini dakika 90 ziliihakikishia nafasi Real Madrid.

Kipigo cha Liverpool na kocha wa wakati huo, Brendan Rodgers aliyeweka kikosi dhaifu, kiichangia kufungwa kwa timu hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24 katika msimu uliopita.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
 Rodgers alimpumzisha nahodha wa England Steven Gerrard pamoja na mchezaji mwenzake wa timu hiyo Raheem Sterling na Jordan Henderson, pamoja na mchezeshaji Mbrazil Philippe Coutinho.

Liverpool ilifungwa bao 1-0 na kukawa na tetesi kuwa Rodgers aliisaliti historia na utamaduni wa klabu hiyo ambayo imeshinda taji hilo mara tano na kuwaangusha maelfu wa mashabiki wa timu hiyo.

Kwa upande wa mabingwa watetezi Real Madrid, wenyewe walifika mapema kuendelea na mazoezi hapa Kiev kwa ajili ya mchezo huo wa leo Jumamosi wakati mabingwa hao mara 12 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakitaka kutetea taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Hatahivyo, Real Madrid wasitarajie mteremko kwa Liverpool iko vizuri na ina safu kali ya ushambuliaji, ambayo imetoa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika Ligi Kuu ya England msimu uliomalizika.

Raphael Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric, Toni Kroos, Isco, Cristiano Ronaldo na Benzema wataanza katika kikosi cha kwanza. Gareth Bale atakuwa katika benchi lakini akitarajia kuingia wakati wowote.
 
Mchezaji bora wa msimu, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane watakuwa katika safu ya ushambuliaji wakati wakijaribu kuishtua Real Madrid wakirejea walivyofanya mwaka 2014.

Salah, Firmino na Mane wana magoli 29 kati yao msimu huu katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na jumla wana mabao 90 wakati wakitengeneza utatu mtakatibu katika ushambuliaji huku kocha wao Klopp akiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi leo Jumamosi.

Yanga Wanusurika Kupapaswa na Ruvu Shooting


Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wazamani wa Soka Tanzania Bara, Yanga jana walinusurika kupapaswa na Ruvu Shooting katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kulazimishwa sare ya kufungana 2-2.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa imefikisha pointi 52 ikiendelea kuwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC iliyopo katika nafasi ya pili na Simba inayoongoza na tayari imeshatwaa ubingwa.

Yanga waliandika bao la kwanza katika dakika ya 17 lililofungwa na Matheo Anthony baada ya kuunganisha  kifundi krosi ya Pappy Shishimbi.

Yanga waliutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza na kulishambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara, lakini walikosa mabao mengi baada ya kushindwa kutumia nafasi kibao walizopata.

Vijana wa Ruvu Shooting walipambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa penalti iliyowekwa kimiani na Hamis Mcha baada ya beki wa Yanga, Abdallah shaibu kuushika mpira katika eneo la hatari.

Yanga nusura wafunge bao la pili katika dakika ya 33 wakati Kamusoko alipokuwa katika nafasi nzuri ya kufunga, lakini shuti lakini liligonga mtambaa panya na mpira kurudi uwanjani na kuokolewa.

Baada ya mashambulizi ya hapa na pale,Yanga walifanikiwa kuandika bao la pili lilifungwa na Maka Edward kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Tshishimbi.

Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kiloanza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu, lakini Ruvu Shooting ndio walikuwa na bahari baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika ya 49 kwa bao lililowekwa kimiani na Issa Kanduru.

Full Maganga alipoteza nafasi ya wazi kuifungia Rivu Shooting bao la ushindi, lakini akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, alipiga shuti lililokwenda nje ya lango na kuikosesha timu yake bao.

Vikosi vilikuwa; Yanga: Ramadhani Kambwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma, Maka Edward, Pius Buswita, Papy Tshishimbi, Matheo Anthony, Thabani Kamusoko na Emmanuel Martin.

Ruvu Shooting: Abdallah Rashid, George Aman, Yusuf Nguya, Amissi Kisanga, Rajabu Zahir, Baraka Mtui, Abrahman Mussa, Shaban Msala, Issa Kanduru, Fullu Maganga na Amissi Mcha.

Thursday 24 May 2018

DStv Kutangaza Kombe la Dunia Kwa Kiswahili

Wadau mbalimbali wa michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface (watatu kushoto) wakipata futari jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimebaki siku kadhaa kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, Kampuni ya Mult-Choice kupitia king’amuzi chake cha DStv, itatangaza mechi zote za Kombe la Dunia kwa lugha ya Kiswahili.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua  wa mashindano hayo, Mkuu wa Uendeshaji wa Mult’Choice Tanzania Ronald Selukindo alisema kuwa wametenga chaneli sita, ambazo zitakuwa maalum kwa Kombe la Dunia, ambalo linaanza Urusi kuanzia Juni 14 hadi Julao 15.
Alisema chaneli hizo zote zitaonekana kwa kiwango cha hali ya juu, ambacho ni cha HD, ambacho kitawawezesha wateja kuona mechi zote za Kombe la Dunia kwa picha zenye ubora wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT), Muhidin Ndolanga (wa pili kushoto) wakati wa kufuturu futari iliyoandaliwa na MultChoice Tanzania jana katika hoteli ya Serena.
 
“Hii ni zaidi ya ofa” alisema Ronald Shelukindo, “Sasa tunataka Watanzania waweze kupata burudani ya Kombe la Dunia 2018 kwa namna tofauti kabisa. Kwanza kwa wateja wapya wataweza kujiunga kwa Sh 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure!” alisema Shelukindo.

Pia alisisitiza kuwa mbali na kutangaza kwa kugha ya Kiswahili kwa kutumia watangazaji wa michezo waliobobea wa hapa nchini pamoja na wachambuzi wake, ambao watakuwa nchini wakitangaza na kuchanbua mechi hizo kwa Kiswahili.
 

Alisema pia wateja wa DStv sasa wataweza kutazama chaneli hizo popote kupitia katika simu zao za mkononi, na tablet
Akitoa maelezo kuhusu jinsi DStv ilivyojizatiti kuwahakikishia Watanzania burudani isiyo na kifani msimu huu wa Kombe la Dunia, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Alpha Mria, amebainisha kuwa DStv itaonesha michuano hiyo katika vifurushi vyake vyote,
 “Kwakeli msimu huu wa Kombe la Dunia, kila atakayekuwa na DStv atakuwa anapata kile anachostahili, kwani mechi zote zitaonekana live, kwenye HD na kwenye vifurushi vyote, huku pia zikitangazwa kwa lugha mbalimbali, ikiwemo lugha ya Kiswahili,” alisema Alpha.
Alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha kila mtu anapata matangazo kupitia lugha anayoitaka kama Kifarasa, Kiingereza na lugha zingine ikiwemo lugha adhimu ya Kiswahili.
 “Tumejipanga, kuwapa Watanzania burudani ya aina yake msimu huu wa Kombe la Dunia,” alisisitiza Alpha.
Katika uzinduzi huo, DStv iliwatambulisha rasmi watangazaji wa soka, ambao watakuwa wakiwaletea Watanzania matangazo ya Kiswahili, ambao ni Aboubakary Liongo, Maulid Kitenge, Ephaim Kibonde, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud - Maestro na Oscar Oscar.
Wakiongea baada ya kutambulishwa, watangazaji na wachambuzi hao mahiri wa soka wamesema wamejizatiti kikamilifu kuhakikisha kuwa wanawaletea matangazo na uchambuzi wa kina ili kuhakikisha kuwa kila mpenda soka anafurahia na kuyaelewa vizuri mashindano hayo.

Aidha, MultChoice ilifurisha wadau mbalimbali wa michezo jana jioni katika hoteli ya Serena kabla ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa Kombe la Dunia 2018 kwa kiswahili.