MOSCOW, Russia
WANAUME wawili wanashikiliwa na vyombo vya usalama kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani wa Russia Boris
Nemtsov, taarifa kutoka Makao Makuu ya Usalama (FSB) imeeleza.
Anzor Gubashev na Zaur Dadayev, wote kutoka mkoa wa Caucasus,
walikamatwa Jumamosi, alisema mkurugenzi wa FSB Alexander Bortnikov.
Wapelelezi wa Russia walisema kulikuwa na mipango ya kufanya
mauaji hayo.
Mauaji hayo katika eneo maarufu la darajani ndani ya
eneo hilo la kiistoria la Kremlin yalishtua Russia.
Naibu Waziri Mkuu wazamani na mwasiasa mkongwe huyo
mwenye umri wa miaka 55, alipigwa risasi mgongoni mara nne usiku wa Februari 27
wakati akitembea mtaani na rafiki yake wakike.
Mwanasiasa huyo alizikwa Jumanne jijini hapa.
Taarifa hiyo imetolewa na televisheni ya taifa na mkuu
wa FSB mwenyewe ikiwa ni alama ya wazi kuwa Kremlin anataka kuonekana
akilichukulia jambo hilo kwa makini zaidi.
Bwana Bortnikov hakutoa taarifa zaidi jinsi watuhumiwa
hao wanayoshikiliwa, katika taarifa yake fupi iliyotolewa na televisheni
inayomilikiwa na taifa ya Channel One, lakini alisema kuwa uchuguzi ulikuwa
bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment