Saturday, 7 March 2015

Yanga, Simba nani kulala mapema kesho? *Azam FC kuikaribisha JKT Ruvu

Kikosi cha Yanga Africans.
Na Mwandishi Wetu
PATASHIKA nguo kuchanika kesho wakati watani wa jadi wa Yanga na Simba watakapovaana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Huo ni mchezo wa marudiano wa timu hizo baada ya ule wa kwanza uliofanyika katika duru la kwanza kutoka sare.

Timu hizo zinachuana wakati Yanga wakiwa kileleni baada ya kujikusanyia pointi 31 huku wenzao wa Simba wakiwa katika nafasi ya nne baada ya kuwa na pointi 23 baada ya michezo 16. Yanga wamecheza mechi 15.

Kikosi cha Simba Sports Club.
Simba wako kambini Zanzibar na wenzao Yanga wamejichimbia mjini Bagamoyo katika Chuo cha Uvuvi Mbegani, ambapo timu zote zimetamba kuibuka na ushindi.

Kitakwimu, Yanga wako vizuri zaidi kwani katika mechi za hivi karibuni wameshinda michezo mingi ukilinganisha na wenzao wa Simba, ambao ukiondoa mechi dhidi ya Prisons hivi karibuni, wamekuwa hawafanyi vizuri.

Yanga katika hali ya kuonesha wako vizuri zaidi, wiki iliyopita walizifunga Tanzania Prisons na Mbeya City katika mchezo wa ligi hiyo kwenye Uwnja wa Kumbukumhu ya Sokoine mjini Mbeya.

Mechi zingine kesho Jumapili ni Mgambo JKT wataikaribisha Ndanda FC na Mtibwa Suga dhidi ya Mbeya City.

Aidha, ligi hiyo itaendelea leo katika viwanja tofauti wakati Polisi Moro itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting huku Coastal Union ikicheza na Kagera Sugar, JKT Ruvu watatoana jasho na mabingwa watetezi Azam FC.

Msimamo:
                 MP  W   D   L   GF  GA  +/- Pts
1Young Africans  15  9   4   2   21  8   13  31 
2 Azam   FC      15  7   6   2   22  12  10  27 
3 Kagera Sugar   17  6   6   5   13  13   0  24 
4 Simba SC       16  5   8   3   20  12   8  23 
5 Mtibwa Sugar   16  5   7   4   17  16   1  22 
6 Coastal Union  17  5   7   5   11  10   1  22 
7 Ndanda         17  6   4   7   16  19  -3  22 
8 Stand United   17  5   6   6   16  18  -2  21 
9 Ruvu Shooting  17  5   6   6   12  14  -2  21 
10JKT Ruvu       16  5   5   6   14  15  -1  20 
11Polisi Moro    17  4   7   6   13  16  -3  19 
12Mbeya City     16  4   6   6   11  15  -4  18 
13Mgambo JKT     15  5   2   8   8   16  -8  17 
14 Prisons       17  1   10  6   10  20  -10 13

No comments:

Post a Comment