Monday, 16 March 2015

Sunderland wamtupia virago kocha wao Gus PoyetLONDON, England
KLABU ya Sunderland imemtupia virago kocha wake Gus Poyet baada ya kuiwezesha timu hiyo kushinda mchezo mmoja tu kati ya 12 ya Ligi Kuu ya England inayoendelea.

Timu hiyo inayojulikana pia kama Paka Weusi iko pointi moja juu ya ukanda wa kushuka daraja baada ya Jumamosi kupokea kipigo cha mbwa mwizi cha bao -0 kutoka kwa Aston Villa tena kwenye uwanja wao wa nyumbani.

"Uzuni, hatujaweza kupiga hatua yoyote iliyotegemewa na hata mmoja wetu msimu huu, alisema mwenyekiti wa klabu hiyo Ellis Short.

"Tunajikuta tukipambana, kwa mara nyingie tena, hatimaye tutakuwa na mwisho mbaya chini ya msimamo wa ligi. Tumefanya uamuzi mgumu ambao ulikuwa ukihitajika kwa ajili ya mabadiliko.

Taarifa hiyo ya Sunderland iliendelea kueleza kuhusu mbadala wa Poyet atakayechukua mikoba ya kocha huyo.

Timu hiyo Jumamosi itakuwa na safari ya kwenda West Ham kabla ya kucheza na wapinzani wake wa mji Newcastle Aprili 5 mwaka huu.

Poyet, 47, Jumatatu alikuwa na mazoezi na wachwzaji wa timu hiyo asubuhi lakini baadae alikutana na Mtendaji Mkuu Margaret Byrne na wajumbe wengine wa bodi kujua hatma yake.

Poyet aliichukua timu hiyo kutoka kwa Paolo Di Canio Oktoba mwaka 2013 klabu ikiwa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Lakini baada ya sare nne kutoka katika mechi zao sita za mwisho, iliisaidia timu hiyo kukwepa janga la kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment