LONDON, England
BONDIA wa uzito wa juu Joe Joyce (pichani), ameongeza harakati
zake za kutaka kufuzu kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Rio
mwakani baada ya kushinda mara ya tano katika mfululizo wa mashindano ya
ndondia ya dunia (WSB).
Bingwahuyo wa medali ya dhahabu ya Jumuiya ya Madola
alipata ushindi wa pointi nyingi katika pambano lake dhidi ya Mmorocco Abdeljalil
Abouhamda katika ukumbi wa York jijini hapa.
Ushindi huo umemuacha Joyce,mwenye umri wa miaka 29, kileleni
katika kundi lake la kufuzu la WSB, ambapo akimaliza wa kwanza atakuwa amepata
nafasi ya kwenda Rio mwakani.
Licha ya ushindi wa Joyce, Muingereza Lionhearts alikwenda
chini kwa Mmorocco Atlas Lions kwa 3-2.
"Wapinzani wangu wakubwa watapigana wenyewe mwisho
mwa wiki hii na matokeo sahihi ina maana nitaendelea kubaki kileleni katika
viwango, " alisema Joyce.
Pambano lijalo la Lionhearts litakuwa ugenini dhidi ya Algeria
Desert Hawks litakalofanyika Ijumaa Machi 27.
No comments:
Post a Comment