LONDON, England
MABINGWA watetezi
Real Madrid watakutana na wapinzani wao wa jiji Atletico Madrid katika mchezo
war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ikiwa ni marudio ya fainali ya
msimu uliopita.
Timu ya Ufaransa
ya Paris St-Germain ambayo iliifunga Chelsea katika hatua ya 16 bora itakuwa na
kibarua kigumu pale itakapocheza na Barcelona, ambayo iliwafunga mabingwa wa
Ligi Kuu ya England Manchester City.
Monaco,
iliyoifungisha virago Arsenal kwa faida ya bao la ugenini, imepangiwa kucheza
na Juventus, wakati mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watakabiliana na Porto.
Mechi za kwanza za
hatua hiyo ya robo fainali zitapigwa kati ya Aprili 14-15 April, huku mapambano
ya marudiano yatachezwa Aprili 21-22.
Real Madrid
ilitwaa taji lake la 10 la Ulaya baada ya kuwafunga katika fainali mabingwa wa
Hispania Atletico kwa bao 4-1 katika
muda wa nyongeza katika mchezo uliochezwa Lisbon nchini Ureno msimu uliopita.
Ratiba Kamili:
Paris St-Germain v
Barcelona
Atletico Madrid v
Real Madrid
Porto v Bayern
Munich
Juventus v Monaco
TAREHE ZA ROBO FAINALI:
Aprili 14:
- Atletico Madrid vs Real Madrid, Juventus vs Monaco
Aprili 15:
- PSG vs Barcelona, Porto vs Bayern Munich
Aprili 21:
Barcelona vs PSG, Bayern Munich vs Porto
Aprili 22:
- Real Madrid vs Atletico Madrid, Monaco vs Juventus
Head-to-head
PARIS
SAINT-GERMAIN
Walizifunga timu gani hadi kufikia hatua hii?
PSG ilimaliza ya
pili katika kundi la F nyuma ya vinara Barcelona,ikishinda mara nne katika
mechi zake, ikitoka sare na Ajax na kufungwa na Barca. Walicheza na Chelsea
katika hatua ya 16 bora, ambapo walitoka 1-1 katika mchezo wa kwanza kabla ya
kutoka sare ya 2-2 huku ikibaki na wachezaji 10 katika mchezo wa marudiano
jijini London.
Kocha
Laurent Blanc
Mfungaji anayeongoza kwa mabao:
Edinson Cavani - 6
Wamewahi kutwaa
taji hilo?
Hapana.
BARCELONA
Walizifunga timu gani hadi kufika hapa?:
Barcelona walimaliza
kileleni katika Kundi F, wakishinda mechi tano kati ya mechi zao walizocheza na
walipoteza kwa kufungwa 3-2 dhidi ya PSG. Walicheza na Manchester City katika
hatua ya 16 bora, wakishinda 2-1 kwenye uwanja wa Etihad na 1-0 kwenye uwanja
wao wa Nou Camp.
Walitinga robo fainali
kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-1.
Kocha
Luis Enrique
Mfungaji
anayeongoza kwa mabao
Lionel Messi - 8
Wamewahi kutwaa taji hilo?
Ndio, Mara nne (ushindi
wa pili mara tatu)
--
Kukutana:
Timu hizi
zimekutana mara mbili kabla ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Timu
hiyo ya Ufaransa ilisonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2 mwaka 1995, wakati
Barcelona walisonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini mwaka 2013 (baada ya
matokeo ya jumla kuwa 3-3).
Barcelona haijawahi kushinda mara tatu
ugenini walipocheza na PSG (L2 D1), ikiwemo kufungwa 3-2 mwaka huu katika hatua
ya mtoano
PSG ilifugwa mara moja na kutoka sare mara
mbili katika ya mechi zao tatu za ugenini walizochezea Nou Camp kukabiliana na Barca,
ikiwemo kufungwa 3-1 mwaka huu katika hatua ya makundi.
Timu zote zimefunga katika mechi sita kati
ya saba walizocheza huko nyuma kati ya timu hizo katika mashindano ya Ulaya.
Mechi pekee ambayo hakuna timu iliyofunga bao ilikuwa mwaka 1997 katika fainali
ya Kombe la Washindi, huku Barcelona ikishinda 1-0.
Lionel Messi amefunga mabao matatu katika
mechi nne za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya wapinzani wao hao wa Ufaransa,
wakati Neymar pia alifunga katika mechi zote za hatua ya makundu dhidi yao
msimu huu.
Barca imepoteza mchezo mmoja tu kati ya 11
iliyopita dhidi ya wapinzani wao hao wa Ufaransa, na sasa wanakutana tena msimu
huu.
-
ATLETICO MADRID
Walizifunga timu
gani hadi kufika hapa?
Atletico walimaliza
kileleni mwa msimamo wa Kundi A,
wakishinda mechi nne, wakitoka sare mara moja
na Juventus na kushindwa nyingine 3-2 dhidi ya Olympiacos.Walicheza na Bayer
Leverkusen katia hatua ya 16 bora, wakifungwa ugenini 1-0 lakini walishinda kwa
idadi kama hiyo nyumbani. Walikwenda katika muda wa nyongeza na baadae penati.
Kocha
Diego Simeone
Mfungaji
anayeongoza kwa mabao
Mario Mandzukic -
5
Wamewahi kutwaa taji hilo?
Hawajawhi (wamewahi
kuwa washindi wa pili)
REAL MADRID
![]() |
Baadhi ya wachezaji wa Real Madrid. |
Walizifunga timu
gani hado kufika hapa?
Real Madrid
ilimaliza ya kwanza katika msimamo wa Kundi B, ikishinda mechi zake zote sita
dhidi ya Basle, Liverpool na Ludogorets. Walicheza na Schalke katika hatua ya
16 bora, wakiifunga 2-0 huko Ujerumani lakini walifungwa 4-3 huko Madrid. Walisonga
mbele katika hatua ya robo fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-4.
Kocha
Carlo Ancelotti
Mfungaji bora
Cristiano Ronaldo
- 8
Wamewahi kutwaa taji hilo?
Ndio, mara 10
(ushindi wa pili mara tatu).
-
Wamekutana mara ngapi?
Atletico Madrid na Real Madrid tayari
wamekutana mara sita msimu huu huku Atleti ikiwa haijafungwa, ikishinda mara
nne (ikiwemo mechi zote mbili za ligi) na kutoka sare mara mbili.
Atletico Madrid imefunga mara moja katika
mechi zote nne walizokutana Ulaya huku wapinzani wake hao wa jadi Real, wakishinda
mara moja tu na kushindwa mara tatu.
Ikiwemo msimu huu, angalau wana uhakika wa
kuiwezesha Hispania kuwa na timu moja katika hatua ya robo fainali angalau mara
10 katika kampeni zao.
Mara ya nne tu katika historia ya
mashindano hao ya Ulaya, mchezo wa robo fainali utazikutanisha timu mbili za
Hispania; hatahivyo huu ni msimu wa pili mfululizo hilo kutokoea (Real Madrid v
Sevilla mwaka 1958 na Atletico v Barcelona mwaka 2014).
PORTO
Walizifunga timu gani hadi kufika hapo?
Porto ilimaliza
kileleni katika msimamo wa Kundi H, ikishinda mara nne kati ya mechi zake na
kutoka sare mara mbili. Ushindi wao wa kukumbukwa zaidi ule walipoifunga BATE
6-0 katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi. Pia waliwafunga 3-0 ugenini.
Walicheza na Basle katia hatua ya 16 bora, walitoka sare ya 1-1 na ugenini
kabla ya kushinda 4-0 nyumbani na kupata ushindi wa jumla ya mabao -1.
Kocha
Julen Lopetegui
Mfungaji bora
Jackson Martinez na
Yacine Brahimi – wote wamefunga 5
Wamewahi kutwaa taji hilo?
Ndio, Mara mbili
BAYERN MUNICH
Walizifunga timu gani hadi kufika hapa?
Bayern walimaliza
kileleni katika msimamo wa Kundi E,walishinda mechi tano kati ya mechi
walizocheza na kupoteza mara moja dhidi ya Manchester City. Ushindi wao mnono
ulikuwa dhidi ya Roma, baada ya kuifunga bao 7-1 huko Italia. Walicheza na Shakhtar
Donetsk katika hatua ya 16 bora, walitoka suluhu ugenini lakini walishinda 7-0
nyumbani.
Kocha
Pep Guardiola
Mfungaji bora
Thomas Muller - 5
Wamewahi kutwaa taji?
Ndio mra tano (washindi
wa pili mara tano).
Walipokutana
Bayern ilipoteza mara moja tu kati ya mechi
22 ya mashindano walizokutana dhidi ya timu hiyo ya Ureno (ushindi mara 13, sare
nane): fainali ya Kombe la Ulaya mwaka 1987: 1-2 dhidi ya Porto.
Bayern walishinda katika hatua ya mwisho ya
mtoano walipocheza dhidi ya timu hiyo ya Ureno 12-1: 5-0 ugenini na 7-1 nyumbani
dhidi ya Sporting katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2008/09.
Ushindi pekee wa Porto katika hatua ya
mtoano ya mashindano ya Ulaya dhidi ya timu za ujerumani ulipatikana mwaka 1987
katika fainali; walitolewa katika mechi tatu za mtoano tangu wakati huo, mbili
dhidi ya Bayern n moja dhidi ya Schalke.
Bayern Munich wameshinda mechi saba kati ya
tisa walizokutana dhidi ya timu za ureno, kwa ujumla wakifungwa mbili tu.
JUVENTUS
Wamezifunga timu
zipi hadi kufika hapa?
Juventus walimaliza
wa pili katika Kundi A, wakishinda mechi tatu, wakitoka sare moja na Atletico na
wakipoteza nyingine dhidi ya Olympiacos. Walicheza na Borussia Dortmund katika
hatua ya 16 bora, wakishinda 2-1 nyumbani na kuwafunga Wajerumani 3-0 ugenini
na kushinda kwa jumla ya mabao 5-1.
Kocha
Massimiliano
Allegri
Mfungaji
anayeongoza
Carlos Tevez - 6
Wamewahi kutwaa
taji hilo?
Yes. Mara mbili mara
tano wamemaliza wa pili).
MONACO
Wamezifunga timu
zipi hadi kufika hapo?
Monaco walimaliza
wa kwanza katika Kundi C, wakishinda mechi tatu, wakitoka sare mara mbili dhidi
ya Benfica. Walicheza na Arsenal katika hatua ya 16 bora na kuifungasha virago
kwa jumla ya bao 3-1 ugenini kabla ya kufungwa 2-0 nyumbani na kusonga mbele.
Kocha
Leonardo Jardim
Mfungaji
anayeongoza;
Lucas Ocampos,
Aymen Abdennour, Yannick Ferreira-Carrasco, Dimitar Berbatov, Geoffrey
Kondogbia, Fabinho, Joao Moutinho – wote
kila mmoja amefunaji bao moja.
Wamewahi kutwaa
taji hilo?
Hawajawahi
(wameishia namba mbili).
Mara walizokutana:
Timu hizo mbili zimekutana mara moja tu
kabla ya msimu wa mwaka 97/98 katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wakati Juventus
waliposhinda 4-1 nyumbani na kupoteza kwa bao 2-3 huko Monte Carlo wakati
wakielekwa katika fainali ambako walifungwa 1-0 na Real Madrid.
Walipokutana na timu za Ufaransa katika
mashindano ya Ulaya mara 24 pamoja na timu za Ufaransa (ikiwemo Intertoto), kibibi
hicho cha Turin kikipoteza mara tano, kikishinda mara 14 na kutoka sare mara
tano.
Hatahivyo katika
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Juve imeshinda mara mbili kati ya sita dhidi ya timu
za Ufaransa (moja ilishinda dhidi ya Monaco mwaka 1998 na ilishinda dhidi ya Nantes
mwaka 1996).
Katika mechi za Ulaya walizokutana mara 11
na timu za Italia, Monaco ilishinda mara tatu (sare mara mbili na kufungwa mara
sita), ingawa ushindi wa mechi mbili kati ya hizo ulikuja katika mechi zao tatu
walizocheza mara ya mwisho na timu hiyo ya Serie A.
No comments:
Post a Comment