![]() |
Umati wa watu ukishuhudia ajali hiyo. |
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WATU 43 wamefariki
dunia katika ajali ya gari iliyotokea Iringa baada ya basi la Majinja Express
lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kugongana na lori na
kuanguangukiwa na kontena.
Kwa taarifa
zilizopatikana katika eneo la tukio, watu 37 walifariki papo hapo na wengine
sita walifariki katika hospitali ya Mufindi mkoani Iringa akiwemo mwanafunzi
mmoja.
Huzuni kubwa
ilitawala katika mji mdogo wa Mafinga baada ya ajali hiyo huku wasamaria wema
wakijitahidi kuondoa miili ya waliokufa, na kuwakimbiza hospitalini majeruhi.
Ajali hiyo
ilihusisha lori lenye namba T689 APJ likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa
jina la Maka Sebastian (26)mali ya CIPEX Company huku basi likiwa na namba T438
CDE likiendesha na dereva Baraka Gabriel (37).
Habari
zisizothibitishwa zinasema kuwa mekana wengi wao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam waliokuwa wakitokea jijini Mbeya kati ya hao walofariki ni
wanaume 33 wanawake 7, watoto 3 na majeruhi 22.
Mmoja wa abiria wa
basi hilo,Musa Mwasege akisimulia chanzo cha ajali hiyo alisema kuwa chanzo
ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi
alilopanda kwa kuwa katika mwendo kasi licha ya ubovu wa barabara hiyo kuwa na
mashimo mengi yanayosababisha ajali.
“Sehemu
iliyotokea ajali kwa kweli ni mbovu hivyo dereva wetu baada ya kupunguza mwendo
akawa anazidi kuongeza na kutumbukia katika shimo na
kusababisha kugongana uso kwa uso na roli hilo na kisha kontena kutuangukia
baada ya hapo sikutambua lolote hadi nilipofika hospitali,”
alisema.
Kwa upande wake
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akizungumza katika eneo la ajali alisema
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni ubovu uliokithiri wa barabara hiyo na ni tukio la
kuhuzunisha sana kwa Watanzania na kuagiza wakala wa barabara kuanza
matengenezo ya barabara hiyo mara moja.
Kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amekiri kutokea kwa ajali hiyo na
kusema kuwa chanzo cha ajali ni ubovu wa barabara kutokana kuwa na mashimo
mengi.
Kamanda Mungi
aliwataja abiria waliokuwemo katika basi hilo kuwa ni Esta Emanuel Lusekelo,
Jerimiah Wakison, Doto Katuga, Diga Solomon, Theresia Kaminyage, Frank
Chiwango,
Luteni Sanga, Alfred Sanga, Juliana Bukuku, Esta Fide na Paulina Justin.
Wengine ni
Catherine Mwajengi, Zira Kasambala, Rebeka Kasambala, Mbamba Ipyana, Dulile
Kambala, Frank Mbaule, Mustapha Ramadhan, Bwana Mussa, Shadrak Msigwa, Mathias
Justin, na mwingine alijulikana kwa jina moja la Elias.
Naye mganga Mkuu Mfawidhi
wa hospitali ya wilaya ya Mufindi Boaz Mnenegwa alikiri kupokea maiti 37 na
majeruhi 22 zilizotokana na ajali hiyo na kusema kuwa majeruhi watano
walifariki mara baada kufikishwa hospitalini hapo.
Alisema kuwa
kutokana ufinyu wa nafasi katika chumba cha kuhifadhia mahiti hospitalini hapo
maiti 32 zilipelekwa katia hospitali ya rufaa ya Iringa kwa ajili ya
kuhifadhiwa.
No comments:
Post a Comment