![]() |
MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa Bayern Munich
Mhispania Pep Guadiola amekiri kuwa hatma ya kibarua chake iko shakani endapo
timu hiyo itashindwa kufuzu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Guardiola alikiri
kuwa huenda akapoteza kazi yake endapo Bayern Munich watafungwa na Shakhtar
Donetsk katika mchezo wa Jumatano wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Bayern inapewa
nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali kufuatia sare ya bila
kufungana katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ukraine, licha ya kumpoteza
mchezaji wao Xabi Alonso aliyetolewa nje.
Hatahivyo, Guardiola
ianajua vizuri matarajio ya wapenzi wa timu hiyo katika mchezo utakaofanyika
kwenhe uwanja wa Allianz Arena, na anaamini kuwa hata kucheza fainali ya
mashindano hayo bado hakumuhakikishii kuendelea kuwepo klabuni hapo.
Alisema wakati wa
mkutano wake kabla ya mechi: "Bado mimi ni kijana mdogo, lakini najua nini
kitatokea endapo hatutavuka hatua hii na kucheza hatua inayofuata.
"Mimi ni
kocha wa klabu kubwa kweli kweli na ninajia ni shida endapo hatutasonga mbele
katika robo fainali au nusu fainali, au hata fainali. Hiyo ni sehemu ya kazi
yangu na ninajiandaa kwa hilo."
No comments:
Post a Comment