Wednesday, 25 March 2015

Vincent Enyeama afikisha mechi ya 100 Super EaglesLAGOS, Nigeria
NAHODHA na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama (pichani), ameingia katika historia baada ya kucheza mechi ya 100 lakini Uganda `The Cranes ilitibua sherehe hiyo baada ya kuifunga Super Eagles bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Akwa Ibom huko Uyo.

Enyeama amekuwa mchezaji wa 23 wa Afrika na Mnigeria wa pili katika soka kufikicha mechi ya 100 katika historia yake ya kucheza mchezo huo.

Kipa huyo anayeidakia klabu ya Lille sasa anajiunga katika orodha ya wachezaj mahiri kama akina Ahmed Hassan, Hossam Hassan, Essam El-Hadary, Rigobert Song, Ibrahim Hassan, Hany Ramzy, Didier Zokora, Geremi, Samuel Eto'o and Kolo Toure, waliofikisha mechi 100 au zaidi kwa kuzichezea nchi zao.

Wengine wenye mechi 100 ni pamoja na Noureddine Naybet, Abdel-Zaher El-Saqua, Wael Gomaa, Ahmed El-Kass, Aaron Mokoena, Joseph Musonda, Radhi Jaidi, Ahmed Fathi, Nader El-Sayed, Didier Drogba, Elijah Tana na nahodha wazamani wa Nigeria Joseph Yobo.

Lakini mchezaji alijikuta akimaliza mechi hiyo kwa majinzi baada ya timu yao kushindwa katika mji aliozaliwa wa Akwa Ibom.

Wakati akielezea kuhusu miaka yake 13 ya kuichezea timu hiyo ya taifa, kipa huy alikiri kupanda na kushuka na wakati fulani hadi alifikia kutaka kuachia ngazi.

"Kwa kweli namshukuru Mungu kwa mafanikio haya. Napenda kuwashukuru Wanaigeria wote kwa mafanikio haya. Lakini ni jambo la kusikitisha kufungwa lakini ndio soka. Timu yetu ina wachezaji wengi wageni, itafanya vizuri baadae.

"Ina maana miaka 13 kuvaa rangi za jezi hii ya taifa sio jambo rahisikulikuwa na kupanda na kushuka, alisema Enyeama.

Enyeama alianza kuichezea timu ya taifa kwa mchezo dhidi ya Harambee Stars ya Kenya mwaka 2002.

No comments:

Post a Comment