Tuesday, 10 March 2015

Mancini amtabiria Yaya Toure kutua Inter MilanLONDON, England
KOCHA wa Inter atafurahi kuungana na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast, aliyesema anafikiria kuondoka Manchester City katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Roberto Mancini anasema kuwa Yaya Toure (pichani) atajiunga na Inter endapo nyota huyo wa Manchester City ataamua kwenda Italia kucheza soka.

Nahodha huyo wa Ivory Coast amebakisha miaka miwili katika kataba wake na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England lakini kuna tetesi kibao kuwa ataondoka Etihad mwishoni mwa msimu wa mwaka 2014-15.

Mancini ambaye ni kocha wazamani wa Man City boss Mancini ametoa siri ya kuungana na kiungo huyo ambaye aliahidi kujiunga na San Siro.

"Ikiwa Yaya Toure atakuja Italia, atajiunga na Inter," alisema kocha huyo wa Nerazzurri.

No comments:

Post a Comment