Thursday, 19 March 2015

`Black Stars' kucheza na Namibia Machi 25ACCRA, Ghana
TIMU B ya wakubwa ya Ghana, the local Black Stars (pichani), itaikaribisha timu A ya Namibia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki Machi 25.

Timu hiyo ya Black Stars ambayo kwa sasa imepiga kambi ikijiandaa kwa mashindano ya Cosafa Cup 2015 yatakayofanyika Mei na yake ya kufuzu kwa ajili ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa nyumbani, yaani Chan mwezi ujao.

Timu hiyo ya Namibia inayojulikana kama Brave Warriors inatarajia kutua Ghana Jumatatu kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa utakaofanyika kwenye uwanja wa Len Clay huko Obuasi.

Mchezaji wa kimataifa wa Namibia Petrus Shitembi, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo vinara wa Ligi Kuu ya Ghana AshantiGold, anatarajia kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki.

Namibia will itaondoka mara baada ya mchezo huo na kwenda Togo kukabiliana na Hawks huko Lome siku tatu baadae.

No comments:

Post a Comment