Sunday, 8 March 2015

Andy Murray aing'arisha Uingereza Davis CupGASGOW, Scotland
ANDY Murray alitinga katika robo fainali ya mashindano ya tenisi ya Davis Cup upande wa timu ya taifa ya Uingereza baada ya kushinda dhidi ya Mmarekani John Isner jijini hapa.

Mchezaji huyo wa Scotland, ambaye katika seti ya kwanza aliokoa pointi tatu, alisonga mbele kwa ushindi wa 7-6 (7-4) 6-3 7-6 (7-4) na kuipatia Uingereza ushindi wa 3-1 na kuongoza katika mpambano wa raundi ya kwanza.

Baada ya ushindi huo, Uingereza sasa itacheza nyumbani na Ufaransa JUlai, huku uwanja ukitangazwa baadae.

"Najisiki vizuri sana. Hii ni juhudi ya timu nzima na ninafikiri kila mmoja anakubali kuwa timu ilitekeleza majukumu yake, " alisema Murray.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye kwa mara ya kwanza wiki hii ndiyo amerejea Scotland katika kipindi cha miaka minne, alionekana kufanya vizuri tangu katika hatua ya kwanza.

"Kwa niaba ya wachezaji wote napenda kuwashukuru mashabiki kwa sababu walifanya hali kuwa nzuri anbayo sijawahi kuiona, " aliongeza mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment