Cristiano Ronald akiwa na Rolls-Royce lake jipya mazoezini |
.MADRID, Hispania
MCHEZAJI Cristiano
Ronaldo alirahisisha ufikaji katika mazoezi ya Real Madrid baada ya kutinga na
gari lake jipya aina ya Rolls-Royce jeupe lenye thamani ya pauni 330,000 (sawa
na Tsh.660,000,000).
Mchezaji huyo bora
wa dunia mara tatu aliondoka katika uwanja wa mazoezi kwa staili ya aina yake
wakati kocha Carlo Ancelotti akiwaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo wa La
Liga dhidi ya Athletic Bilbao utakaofanyika Jumamosi.
Ronaldo alifunga
bao lake la 30 la ligi katika mchezo wa mwisho wa Real Madrid dhidi ya Villarreal,
lakini haikuwazuia kupoteza pointi mbili baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye
uwanja wa Bernabeu.
Zikiwa zimebaki
mechi 12 Ronaldo amebakisha bao moja tu kufikisha yale aliyofunga msimu
uliopita, na nyota huyo wazamani wa Manchester United amekuwa mchezaji wa
kwanza katika historia kutoka katika ligi tano kufunga mabao 30 katika msimu
mmoja kwa mara ya tano mfululizo.
Real Madrid iko
pointi mbili mbele ya Barcelona kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania huku timu
hiyo ikitarajiwa kwenda Nou Camp Machi 22.
Real wanatakiwa
kuifunga Bilbao Jumamosi iliyopo katika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi
hiyo kabla hawajaanza kuelekeza nguvu zao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya siku
tatu baadae.
Watakutana na Schalke
katika mchezo wa marudiano wa timu 16 bora huku Real Madrid wakiwa na faida ya
bao 2-0. Ilikuwa kwenye uwanja wa Veltins Arena huko Ujerumani Februari 18
wakati Ronaldo alipofunga bao la kwanza na kuiweka Real nafasi nzuri ya kufuzu
kwa robo fainali.
No comments:
Post a Comment