![]() |
Kipa Vicent Enyeama akitengeneza sosi lake. |
ABUJA, Nigeria
KIPA wa Nigeria Vincent Enyeama anajiandaa kucheza
mchezo wake wa 100 wa kimataifa baada ya kutangazwa katika kikosi cha Super
Eagles kitakachocheza mchezo wa kirafiki na Bolivia utakaofanyika Machi 26.
Enyeama mwenye umri wa miaka 32 ni miongoni mwa
wachezaji 28 waliochaguliwa kuunda kikosi hicho kilichopo chini ya kocha wa
muda Daniel Amokachi.
Mshambuliaji aliye katika fomu wa West Brom, Brown
Ideye naye yumo katika kikosi hicho, pamoja na Odion Ighalo wa timu ya daraja
la kwanza ya Watford.
Mshambuliaji majeruhi wa Stoke Victor Moses naye pia
yuko katika skwadi hiyo ambaye amemuhakiishia kocha Amokachi kuwa atakuwa fiti
kucheza mchezo huo.
Kikosi hicho cha timu ya taifa ya Nigeria kitakuwa
pamoja na kusafiri kwenda Afrika Kusini kucheza mchezo mwingine wa kirafiki
Jumapili, Machi 29.
Kikosi
Kamili cha Nigeria:
Makipa:
Vincent Enyeama (Lille OSC, Ufaransa); Theophilus Afelokhai (Kano Pillars);
Chidiebere Eze (Ifeanyi Ubah United)
Mabeki:
Chima Akas (Sharks FC); Godfrey Oboabona (Rizespor FC, Uturuki); Azubuike
Egwuekwe (Warri Wolves); Nelson Ogbonnaya (Heartland FC); Kenneth Omeruo
(Middlesbrough FC, England); Akeem Latifu (Aalesunds FC, Norway); Leon Balogun
(Darmstadt 98, Ujerumani).
Viungo:
Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italia); Steven Ukoh (Biel-Bienne FC, Uswisi); Sone
Aluko (Hull City, England); Hope Akpan (Reading FC, England); John Ogu (Hapoel
Be'er Sheva, Israel); Michael Babatunde (Volyn Lutsk, Ukraine); Joseph
Nathaniel (Sharks FC); Kingsley Sokari (Enyimba FC).
Washambuliaji:
Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Aaron Samuel (Guangzhou R&F, China);
Brown Ideye (West Brom, England); Odion Ighalo (Watford FC, England); Anthony
Ujah (FC Cologne, Ujerumani); Moses Simon (KAA Gent, Ubelgiji); Ubong Moses
(Kano Pillars); Stanley Dimgba (Warri Wolves); Mfon Udoh (Enyimba FC); Standby
- Victor Moses (Stoke City, England)
No comments:
Post a Comment