Monday, 16 March 2015

Ricardo Carvalho aionya Monaco kuwa makini na ArsenalMONACO, Ufaransa
BEKI wazamani wa Chelsea amesema kuwa ushindi wa 3-1 wa timu yake katika mchezo wa kwanza sio wakushangaza, lakini anakiri kuwa Monaco bado haijajihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali.

Beki wa Monaco Ricardo Carvalho alisema ushindi wao huo wa 3-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Arsenal hauipi nafasi ama Arsene Wenger au timu yake.

Kabla ya kucheza mchezo wa marudiano Jumanne, Carvalho ambaye alikuwa ameumia katika mchezo wa kwanza, alisema kuteleza kwa Arsenal ni sehemu ya mchezo, na Monaco nao wanaweza kupoteza faida ya kucheza nyumbani katika mchezo huo wa Jumanne.

"Sijui [kama Arsenal wanaidharau Monaco]. Sifikirii hivyo," alisema beki huyo wa kati wazamani wa Chelsea. Wakati fulani hilo hutokea katika soka. Ni kweli, kwa wengi ni jambo la ajabu.

"Arsenal ni timu kubwa, lakini wakati fulani katika soka, ni kweli hilo linaweza kutokea. Hivyo inaweza kutokea tukiwa kwetu nyumbani, kwa sababu katika soka huwa kuna aina kama ya maajabu kama hiyo.

No comments:

Post a Comment