Monday, 9 March 2015

Mali wamtupia virago kocha waoBAMAKO, Mali
MALI imeachana na kocha Henryk Kasperczak (pichani) kufuatia timu hiyo kufanya vibaya katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Shirikisho la Soka la Mali lilisema kuwa, baada ya kikao na kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 raia wa Poland "imekubaliwa kuwa tusiongeze mkataba wake".

Kasperczak alishindwa kuivusha timu kutoka katika makundi katika mashindano ya hivi karibuni yaliyomalizika Guinea ya Ikweta.

Mali ilimaliza na Guinea lakini ilitolewa baada ya kutofanya vizuri.

Timu hiyo ilipanga kumtangaza kocha mpya Machi 25 huku makocha wazamani Alain Giresse, Stephen Keshi na Patrice Carteron wakiaminika kuwa majina yao yako mbele kujaza nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment