Sunday, 31 May 2015

Ufungaji wa tamasha la michezo la shule za Filbert Bayi ulivyosisimua Mkuza Kibaha

Soka lilipamba moto

Soka ilikuwa kivutio pia katika tamasha hilo la michezo ambalo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.

Ushindi mtamu!: Ofisa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Mwinga Mwanjala (kulia) akifurahia na mwalimu bao lililofungwa na timu ya shule ya msingi ya Filbert Bayi ya Kimara dhidi ya wenzao wa Kibaha. Timu hizo zilifungana 1-1.

Wanafunzi wa shule za msingi za Filbert Bayi nao walichuana hata katika soka pia.

Wazazi wenye watoto katika shule za Filbert Bayi wakitoana jasho katika kuvuta kamba.

Mchezo wa kuvuta kamba, haikuwa rahisi kushinda

Mkurugenzi wa shule za Filbert Bayi, Anna Bayi (kulia), akiteta jambo na msaidizi wake Eliberth wakati wa bonanza la michezo la shule hizo lililofanyika Mkuza, Kibaha.Kumekucha mchezo wa kukimbiza kuku; kila mmoja akifikiria kitoweo endapo atamkamata jogoo hilo.Mchezo wa kukimbiza kuku

Mchezo wa kukimbiza kuku uliwatoa jasho washiriki.

Mchezo wa kukimbiza kuku nao ulikuwepo katika tamasha hilo la michezo la shule zaFilbert Bayi.

Timu ya shule ya sekondari ya Filbert Bayi katika picha ya pamoja kabla hawajacheza na wenzao wa East Coast.

Timu ya soka ya shule ya sekondari ya East Coast katika picha ya pamoja.

Mgeni rasmi akikagua timu ya shule ya sekondari ya East Coast ya Pwani kabla haijacheza na Filbert Bayi Mkuza Kibaha.

Mgeni rasmi akiteta jambo na wachezaji wa timu ya shule ya sekondari ya East Coast na wale wa Filbert Bayi kabla ya kuanza kwa pambano la soka. Filbert Bayi walishinda 2-0.

Hata mchezo wa mbio za pikipiki ulikuwepo, mmoja wa waratibu Peter Mwita akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki hao.

Baadhi ya wakuu wa shule za Filbert Bayi wakati wa bonanza la michezo wakiteta jambo.

Uwanja mpya wa ndani wa shule za Filbert Bayi umekamilika na tayari umeanza kutumika wakati ukisubiri kufunguliwa rasmi wakati wowote.


BONANZA la Michezo la Shule za Filbert Bayi lilivyofana Mkuza Kibaha

Kazi! Kazi tu!Hakuna ubosiMwenyekiti wa Bodi ya shule za Filbert Bayi, Bayi akirekebisha vipimo kwa ajili ya mchezo wa kutupa mkuki kabla ya kuanza bonanza la michezo la shule hizo Mkuza Kibaha.
Mwanasheria Kenya atoa ng'ombe, kondoo kumuoa binti wa ObamaNairobi, Kenya

MWANASHERIA wa Kenya ametoa kwa Rais Barack Obama ngombe 50 na vitu vingine vinavyohusiana na mifugo kwa ajili ya mahali ili kumuoa binti wa rais huyo Malia mwenye umri wa miaka 16, taarifa imeeleza.

Felix Kiprono alisema alikuwa yuko tayari kutoa ngombe 50, kondoo 70 nambuzi 30 ili kukamilisha ndoto yake ya kumuoa binti wa kwanza wa rais huyo kutoka taifa kubwa zaidi duniani.

"Tangu mwaka 2008 nilipata nia ya kumuoa Malia, " alisema, katika mahojiano na gazeti la Nairobi.

Wakati akipata nia hiyo, Rais Obama ndio kwanza alikuwa katika harakati za kutaka kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza huku Malia wakati huo akiwa na umri wa miaka 10.

"Ukweli ni kwamba, toka wakati huo sijawahi kutongoza msichana yeyote na niliahidi kuwa mwaminifu kwake. Nilishauriana haya na familia yangu na walisema wako tayari kunisaidia kuongeza mahali, " alisema.

Kiprono alisema anatarajia kumueleza Obama kuhusu suala hilo na ni matumaini yake kuwa, rais huyo atakwenda Kenya na binti yake huyo wakati mwezi ujao atakapoitembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu awe rais wan chi hiyo, nchi ambayo baba yake alikozaliwa.

Bibi yake Obama ambaye ni Mkenya, ambaye mapema miaka ya 90, bado anaishi huko Kogelo, magharibi ya Kenya, ambako kuna ndugu kibao wa rais huyo.

"Kwa sasa ninaandika barua kwa Obama nikiomuomba aongoxzane na Malia katika zira yake hiyo ya Kenya. Nategemea ubalozi utawasilisha barua hiyo kwa rais huyo," alisema.

Kiprono alikanusha kuwa anataka kumuoa binti huyo kwa lengo la kufuata utajiri.

"Watu huenda wakasema naenda katika familia hiyo kwa lengo la kufuata utajiri, pesa za familia hiyo, lakini hilo sio sababu. Nina mapenzi ya dhati, " alisisitiza.

Mwanasheria huyo kijana, ambaye umri wake haukuwekwa bayana, alisema tayari ameshapanga mipango yake ndoa hiyo itafungwa kimila,ambapo shampeni itakuwa ni maziwa ya mtindi, maarufu kama "mursik".

Kiprono alisema watakapoowa, yeye na binti huyo wa Obama wataishia maisha ya kawaida tu.

"Nitamfundisha Malia jinsi ya kukamua ngombe maziwa, kupika ugali na kuandaa vyakula vingine vya kiasili kama mwanamke yeyote mwingine wa Kalenjin woman," he said.

Wednesday, 27 May 2015

Tanzania mwenyeji fainali Mataifa ya Afrika 2019Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF) limeipa Tanzania uenyeji wa kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya iaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.

Uamuzi huo ulifikiwa wakati wa Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CAF uliofanyika jijini Zurich, Uswisi juzi jioni.

Kamati ya Utendaji ya CAF imekubali ombi la Shirikisho la Soka Tanzania la kuwa mwenyeji wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019, ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya CAF.

Tanzania iliwasilisha ombi hilo kwa msaada wa serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya waziri wake, Fenella Mukangara.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema ni heshima kubwa kwa Tanzania kuandaa mashindano hayo ya Afrika.
Kuandaa mashindano ya vijana ya Afrika ni hatua kubwa katika maendeleo ya soka na itafungua milango kuandaa fainali za wakubwa za Mataifa ya Afrika za Afcon mbeleni, alisema Malinzi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali za Afrika, ambapo imejihakikisha nafasi ya kushiriki fainali hizo kama mwenyeji baada ya kusota kwa miaka mingi ikisaka kufuzu.

TFF ilisema kuwa katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizo, Tanzania, mwezi ujao itaandaa mashindano ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha taifa kuelekea fainali hizo za mwaka 2019.

TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.

 Kupitia mashindano haya ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 huko jijini Mwanza yatasaidia kuunda kikosi imara tena cha ushindano cha U17 mwaka 2019,aliongeza Malinzi katika ukurasa wake rasmi wa Twitter.

Malinzi tayari ameelezea mipango kabambe ya TFF ya kuunda kikosi imara kwa ajili ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika Madagascar mwaka 2017.

Kwa sasa, TFF inaendesha program za vijana wenye umri chini ya miaka 13 na 15 kwa ajili ya kupata timu imara za taifa za vijana kwa ajili ya kufuzu kwa fainali hizo za Madagascar 2017, na zile za vijana za Afrika za mwaka 2019.

Timu hizo zitakuwa zikipiga kambi na kucheza mechi kadhaa za kirafi ndani na nje ya nchi zikiwemo nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini.

Katika mkutano huo wa CAF, Niger imepewa uenyeji wa kuandaa fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakaofanyika mwaka 2019.

Maofisa wa Fifa wakamatwa kwa tuhuma za rushwaZURICH, Uswisi
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) utafanyika kesho kama kawaida licha ya kukamatwa kwa viongozi wake saba kwa sabbau ya madai ya kupokea rushwa ya dola za Marekani Milioni 150.

Miongoni mwa viongozi hao waliokamatwa jana asubuhi ni pamoja na makamu wa rais wa Fifa, Jeffrey Webb.

Uchunguzi wa tuhuma tofauti juu ya uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 ulivyopatikana nao pia umeanza.

Lakini pamoja na tuhuma hizo lakini bado fifa imesisitiza kuwa, Urusi na Qatar bado zitaendelea kuandaa fainali hizo.

Sepp Blatter atakabiliana na Prince Ali bin al-Hussein katika uchaguzi huo wa kesho Ijumaa wakati akisaka kipindi cha tano cha kuongoza taasisi hiyo ya soka.

Viongozi saba wa Fifa walikamatwa jana baada ya Idara ya Haki ya Marekani ikitoa mashataka kadhaa dhidi ya viongozi hao kuhusu tuhuma za rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali ya Uswis imesema kuwa maofisa hao walikuwa wakichunguzwa kuhusiana na tuhuma za kupokea rushwa ya mabilioni.

Taarifa hiyo ilisema kuwa walikamatwa na askari wa Uswisi kwa msaada ya Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI pamoja na Wizara ya Haki ya Marekani.

Pia ilisema kuwa maofisa hao tangu mwanzoni mwa miaka ya 1999 hadi sasa wameshachukua fedha ambazo ni sawa na dola za Marekani Milioni 100.

Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alitembelea hoteli hiyo na kukagua lakini hata hivyo alishindwa kusema lolote kuhusiana na tuhuma hizo.

Lakini aliishia kusema kuwa tumeona taarifa hizi katika vyombo vya habari na kwa sasa tunajipanga kuja kutolea tamko.

Katika kamata kamata hiyo maofisa wa Polisi wakiwa wamevalia nguo za kiraia waliingia hoelini hapo na kisha kuchukua funguo na kwenda kwenye vyumba vya walipokuwa wamefikia maofisa hao wa FIFA na kuwakamata.

Wednesday, 13 May 2015

Barcelona yafungwa na Bayern, yatinga fainali Ulaya 
BAYERN Munich, Ujerumani
MABINGWA wa Ujerumani, timu ya Bayern Munich jana usiku ilitupw nje ya mashindano ya ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika mchezo wa pili wa nusu fainali.

Katika mchezo wa awali, Barcelona ilishinda 3-0 na hivyo timu hiyo ya Hispania imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-3.

Barca sasa itamsubiri mshindi wa jumla kati ya Juventus na Real Madrid kwa ajili ya kucheza fainali itakayofanyika baadae mwezi huu.

Katika mchezo wa kwanza, Juventus iliibuka na ushindi wa bao 2-1 ns timu hizo zinakutana leo Jumatano katika mchezo wa marudiano huko Madrid.

ikutane katika fainali. Juve ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza.

Mabao ya Bayern katika mchezo huo wa jana usiku yalifungwa na Medhi Benatia dakika ya saba, Robert Lewandowski dakika ya 59 na Thomas Muller dakika ya 74, wakati ya Barca mabao yake yote yalifungwa na Neymar dakika ya 15 na 29.