Monday, 9 March 2015

Kocha Manchester United alia na Di MariaDi Maria akioneshwa kadi nyekundu baada ya kumvuta mwamuzi.

LONDON, England
KOCHA wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa Angel Di Maria `hatasamehewa kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo war obo fainali wa Kombe la FA dhidi ya Arsenal.

Kiungo wa Argentina alitolewa nje baada ya kupata kadi mbili za njano za haraka haraka wakati timu yao ikipokea kichapo cha 2-1 kwenye uwanja wao wa Old Trafford.

Awali alipewa kadi ya kwanza kwa kujirusha na badae alivuta shati la mwamuzi Michael Oliver na kusababisha kupewa kadi nyekundu.

"nafikiri alimshika mwamuzi na hilo limekatazwa katika kila nchi, hivyo hakuna cha msamaha," alisema Van Gaal.

"Huko Hispania, anajua kuwa huwezi kumshika mwamuzi, lakini hilo pia ni kutokana na jazba yake.

"Tayari nimeshafanya mazungumzo naye, anajua maoni yangu lakini pia itabidi kuangalia katika video."

Mshmabuliaji wazamani wa Manchester United Danny Welbeck alirejea Old Trafford na kufunga bao la pili la ushindi la kipindi cha pili kwa Arsenal.

Mapema, Nacho Monreal aliifungia the Gunners lakini lilifutwa na lile la kusawazisha alilofunga Wayne Rooney kwa kichwa.

No comments:

Post a Comment