Tuesday, 3 March 2015

50 Cent amtabiria ushindi bondi Mayweather*Acheza kamali akitabiri kupigwa kwa Pacquiao

Rapa 50 Cent (kushoto), akiwa na  Mayweather (kulia) mwaka 2007, ataondoka na kitita cha pauni Milioni 1.5 endapo  Pacquiao atashindwa pambano hilo.

NEW YORK, Marekani
RAPA 50 Cent ataweka kiasi cha pauni Milioni 1 katika kamali akimtabilia Floyd Mayweather kumtwanga Manny Pacquiao katika pambano lao litakalofanyika Mei 2.
Pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa litawakutanisha mabondia hao jijini Las Vegas.
Mwanamuziki huyo atashinda kiasi cha pauni Milioni 1 endapo Mayweather atamtwanga Pacquiao katika pambano hilo ghali zaidi duniani.
Floyd Mayweather Jnr anajulikana kwa makali yake lakini kipindi hiki anaweza kukumbana na upinzani mkubwa katika pambano hilo la aina yake.
Endapo Mayweather atafanya kweli katika pambano hilo la Las Vegas, 50 Cent, ambaye jina lake kamili ni Curtis Jackson, ataondoka na kitita cha dola za Marekani Milioni 2.3 (sawa na pauni Milioni 1.5).
Mwaka jana wawili hao waliingia katika malumbano makali wakati 50 Cent alipoahidi kuchangia kiasi cha dola za Marekani 750,000 za msaada endapo Mayweather angewekwa katika kurasa ya kitabu cha Harry Potter.
Uhusiano wa Mayweather na 50 Cent ulikuwa wa kibiashara hadi mwaka 2012 kabla hawajatengana na baadae bondia huyo kuanzisha kampuni yake ya promotion.
Mayweather na Pacquiao wote walianza kambi zao za mazoezi Jumatatu, huko Las Vegas na Los Angeles.
Wawili hao watazungumza na waandishi wa habari mara moja tu kabla ya mpambano wao huo huko Los Angeles Machi 11.

No comments:

Post a Comment