Wednesday 18 March 2015

David Rudisha na wakali wengine kuchuana Ostrava



LONDON, England
BINGWA wa Olimpiki wa mbio za mita 800 David Rudisha, bingwa wa dunia wa kuruka juu Bogdan Bondarenko na bingwa wa mbio za ndani wa mita 400 Pavel Maslak ni miongoni mwa wanariadha wa kwanza kusaini kushindana katika shindano la Golden Spike IAAF World Challenge litakalofanyika Ostrava Mei 26.

Mpambano huo wa 54 utafanyikia kwenye uwanja uliokarabatiwa na utashirikisha michezo mitatu isiyo ya kawaida.

Rudisha atachuana katika mbio za mita 600, mchezo ambao alishindana mwaka jana huko Birmingham, akikimbia moja ya muda wa kasi zaidi katika historia ya mbio hizo.

Nimefurahi sana kuwa na afya nzuri na kuweza kufanya mazoe kama ninavyotaka. Naangalia mbele kufanya vizuri msimu wa mwaka 2015, alisema bingwa huyo wa dunia wa mbio za mita 800 kutoka Kenya ambaye kwa mara ya mwisho alishinda Ostrava mwaka 2010.

Wakati najiandaa kwa ajili ya mashindano ya Dunia Bijingi nchini China, nimefurahi kuanznia msimu wangu Ulaya kwa kukimbia mbio za mita 600 huko Ostrava, alisema.

Bingwa wa mbio za ndani Maslak atashiriki zile za mita 300 huku akivunja rekodi ya Ulaya kwa kutumia 31.56 iliyowekwa mwaka 1998 na Muingereza Doug Walker.

No comments:

Post a Comment