ABUJA, Nigeria
TIMU ya taifa ya Bolivia imefuta mchezo wa kimataifa wa
kirafiki dhidi ya Nigeria uliopangwa kufanyika Machi 26 huko Uyo kwa sababu za
kisalama, imeelezwa.
Rais wa Shirikisho la Soka la Bolovia Carlos Chavez alisema:
"Matatizo ya kijeshi na hali mbaya ya kisiasa huko Nigeria ndiko
kulikoilazimu nchi hiyo kuufuta mchezo huo."
Hatahivyo, viongozi wa Nigeria wamesema kuwa
wamesikitishwa na kitendo hicho kwani kila kitu kilikuwa katika utaratibu mzuri
kwa ajili ya pambano hilo.
Hiyo ikiwa na maana kuwa kipa wa Nigeria Vinent Enyeama
itambidi kusubiri ili kufikisha mchezo wa 100 wa kuichezea timu hiyo ya taifa.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alitarajia kufikisha
idadi hiyo ya mechi wakati wa mchezo huo na Bolivia, baada ya kutangazwa katika
kikosi cha wachezaji 28 wa Super Eagles kilichopo chini ya kocha wa muda Daniel
Amokachi.
Sasa itambidi kipa huyo kusubiri hadi kucheza mchezo
huo wa 100 hadi pale Nigeria itakapojipima nguvu na Afrika Kusini Jumapili ya
Machi 29 labda kama Shirikisho la Soka la Nigeria litatafuta mchezo mwingine
badala ya ule wa America ya Kusini.
Mshambuliaji aliye katika fomu wa West Brom, Brown
Ideye naye yumo katika kikosi hicho, pamoja na Odion Ighalo wa timu ya daraja
la kwanza ya Watford.
Mshambuliaji majeruhi wa Stoke Victor Moses naye pia
yuko katika skwadi hiyo ambaye amemuhakiishia kocha Amokachi kuwa atakuwa fiti
kucheza mchezo huo.
Kikosi hicho cha timu ya taifa ya Nigeria kitakuwa
pamoja na kusafiri kwenda Afrika Kusini kucheza mchezo mwingine wa kirafiki
Jumapili, Machi 29.
Kikosi
Kamili cha Nigeria:
Makipa: Vincent Enyeama (Lille OSC, Ufaransa);
Theophilus Afelokhai (Kano Pillars); Chidiebere Eze (Ifeanyi Ubah United).
Mabeki:
Chima Akas (Sharks FC); Godfrey Oboabona (Rizespor FC, Uturuki); Azubuike
Egwuekwe (Warri Wolves); Nelson Ogbonnaya (Heartland FC); Kenneth Omeruo
(Middlesbrough FC, England); Akeem Latifu (Aalesunds FC, Norway); Leon Balogun
(Darmstadt 98, Ujerumani).
Viungo:
Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italia); Steven Ukoh (Biel-Bienne FC, Uswisi); Sone
Aluko (Hull City, England); Hope Akpan (Reading FC, England); John Ogu (Hapoel
Be'er Sheva, Israel); Michael Babatunde (Volyn Lutsk, Ukraine); Joseph
Nathaniel (Sharks FC); Kingsley Sokari (Enyimba FC).
Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Aaron
Samuel (Guangzhou R&F, China); Brown Ideye (West Brom, England); Odion
Ighalo (Watford FC, England); Anthony Ujah (FC Cologne, Ujerumani); Moses Simon
(KAA Gent, Ubelgiji); Ubong Moses (Kano Pillars); Stanley Dimgba (Warri
Wolves); Mfon Udoh (Enyimba FC); Standby - Victor Moses (Stoke City, England).
No comments:
Post a Comment