Na Seba Nyanga, Morogoro
BONDIA wa ngumi za kulipwa Francis Cheka aliyekuwa
akitumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani amepunguziwa adhabu na sasa
atatumikia kifungo cha nje, imeelezwa.
Cheka alipewa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kumtwanga meneja wake wa baa Bahati Kibanda hivi karibuni.
Cheka kuanzia jana alitakiwa kuanza kutumikia kifungo
hicho cha nje baada ya maofisa huduma kwa jamii kutoka
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia na kufuata
taratibu kwa makosa aliyotenda ili kuhakikisha anatumikia adhabu mbadala kwa jamii
aliyoikosea.
Bondia Cheka alionekana mwenye uso wa furaha akiwa
ndani ya viwanja vya mahakama, ambapo nje walikuwepo ndugu na jamaa zake, akiwemo
mwalimu wake wa masumbwi, Salehe Abdallah au Komando.
Mbali na hao pia alikuwepo mdogo wake ambaye naye ni
bondia, Cosmas Cheka ambao walikuwa wakimsubiri amalize taratibu na kutoka nje.
![]() |
Bondia Francis Cheka. |
Ofisa wa huduma kwa jamii mkoani Morogoro, Yusuph
Ponela
alisema hayo jana mjini hapa mara bondia Cheka
alipoletwa na maofisa wa Magereza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa kwa
ajili ya kukamilisha taratibu kabla ya kuanza kutumikia kifungo hicho cha nje.
No comments:
Post a Comment