Thursday, 30 April 2015

Baba yake Mayweather amponda mpinzani wa mtoto wake


Mayweather alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mwaka 2012.

NEW YORK, Marekani
MANNY Pacquiao hajawa fiti tangu alipopigwa KO na Juan Manuel Marquez mwaka 2013, anasema baba wa Floyd Mayweather na kocha wa bondia huyo.

Na Mayweather Sr (ambaye ni baba wa bondia huyo) anaamini kuwa mtoto wake atamtwanga tena KO Pacquiao watakapokutna katika pambano lenye utajiri mubwa litakalofanyika Las Vegas Jumapili alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.

"Mara unapigwa kama Pacquiao alipopigwa KO na Marquez, kwa muda mrefu huwezi kupigana sana hadi pale itakapotokea tena, " alisema Mayweather Sr.

Mayweather ameshinda mapambano yake yote 47.
"Pambano hili tayari limeshamalizika. Niamini mimi."
Alipoulizwa anafikiri Pacquiao wakati gali alikuwa katika kiwango cha hali ya juu, Mayweather Sr alijibu: "Wakati alipopigwa na Marquez."

Bondia huyo gwiji wa Mexico (Marquiao) mara mbili alipigwa na Pacquiao na alitoka naye sare mara moja kabla hajamtwanga KO katika raundi ya sita katika pambambano lao la nne la mabondia hao.
Mayweather alimtwanga Marcos Maidana katika pambano lake la mwisho katika ukumbi wa MGM Grand mwaka 2014
Gwigi wa Philippine Pacquiao, bingwa wa uzito sita duniani, tangu wakati hu alishinda mapambano yake matatu, ingawa baadhi ya watu wanasema sio mpiganaji mzuri ukilinganisha na huko nyuma.

Hatahivyo, kocha wa Pacquiao kwa miaka 15, Freddie Roach, alisema bondia wake ana kasi vibaya sana wakati huu akijiandaa na pambano hilo dhidi ya Mayweather, ambaye hajapigwa katika mapambano 47 ya kulipwa.

"Manny anajua kuwa KO ni sehemu ya mchezo wa ngumi, " alisema Roach, kocha bora mara saba wa mwaka. "Ikiwa hautaki kupigwa KO, nenda ukafanye kitu kingine na usicheze ngumi.

"Ilikuwa Ko mbaya zaidi dhidi ya Marquez, alikuwa chini kwa muda mrefu. Nilikuwa na wasiwasi aliporuditena katika gym hakukuwa na mabadiliko.

"Lakini Floyd misuli yake imejengeka zaidi na anapiga ngumi pale anapotaka. Hivyo natarajia atataka kumpiga mapema tena kwa KO.

Tuesday, 28 April 2015

Hatimaye wasafirishaji wa dawa za kulevya wauawa Indonesia


Magari ya wagonjwa yakiwa na miili ya watu nane waliuawa kwa kupigwa risasi nchini Indonesia, wakiwemo Waaustralia wawili Andrew Chan na Myuran Sukumaran, yalipopigwa picha yakiwasili katika bandari ya Cilacap kutoka kisiwani ilipo jela walipofungwa watu hao.
 


JARKATA, Indonesia
SERIKALI ya Indonesia usiku wa kuamkia leo imewaua kwa kuwapiga risasi wauzaji nane wa madawa ya kulevya baada ya watu hao kuhukumiwa kifo.

Hukumu hiyo imetekelezwa na kikosi maalum cha kuwapiga wafungwa risasi, licha ya wito kutoka kwa mataifa mbalimbali duniani kutaka watu hao wasinyingwe.

Wafungwa hao walikuwa tisa, lakini kuuawa kwa raia mmoja wa Ufilipino, Mary Jane Veloso, kumecheleweshwa baada ya mwanamke mmoja kujiwasilisha kwa polisi Nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye aliyemhadaa mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya Indonesia.
Andrew Chan (kulia), na  Myuran Sukumaran (kushoto) ambao waliuawa usiku wa kuamkia leo.
Aidha, raia wawili wa Australia Andrew Chan, 31, na Myuran Sukumaran, 33, walinyongwa pamoja na wafungwa wengine sita na kikosi hicho maalum cha kuwaua wafungwa.

Raia hao wa Australia ndio walikuwa wa kwanza kuuawa baada yam lo wa usiku.

Inaelezwa kuwa Chan ambaye aliukumiwa kifo mwaka 2005 kwa kupanga mpango huo unaoitwa `Bali Nine heroin smuggling plot aliukumiwa kifo miaka miwili iliyopita.
Waaustralia wawili waliouawa na kikosi maalum cha kuua wafungwa usiku wa kuamkia leo.
Chan,ambaye mapema mwaka huu gerezani, alibatizwa na kuwa Mkristo alisema kuwa, Sandiford muda mfupi kabla hajahamishiwa katika kisiwa hicho cha mauaji, alitubu dhambi zake.

Alisema kuwa: 'Siogopi kufa lakini anahofia kufa taratibu. Naogopa risasi na naogopa kwa kuwa hakitakuwa kifo cha haraka. '
Sandiford alihukumiwa kifo huko Bali tagu alipopatikana na hatia ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya pauni Milioni 1.6 za cocaine kupitia uwanja wa ndege wa kisiwani mwaka 2012.

Mwanamke Muindonesia ambaye kifo chake kimeahirishwa alisema kuwa alisafirisha dawa hizo ili kuwalinda watoto zake, ambao usalama wao uliuwa hatarini.

Serikali ya Uingereza ilikataa ombo la kumlipia Sandiford ada ya kisheria kwa ajili ya rufaa yake.

Usiku, yalionekana magari ya wagonjwa yakiwa yamebeba majeneza ya Chan na Sukumaran yakiwasili katika 'kisiwa cha kifo' ambako walipigwa risasi na kuuawa.
Picha tofauti zinaonesha jinsi watu waliokumiwa kifo wanavyoandaliwa hadi kuuawa. Picha namba sita inaeleza kuwa, daktari endapo atathibitisha kuwa mfungwa baada ya kupigwa risasi lakini bado ana dalili ya uhai, basi kamanda wa maaskari hao wauaji anammalizia mfungwa huyo kwa kumpiga risasi kichwani kwa kutumia bastola yake.
Familia ya Chan na Sukumaran ilitoa taarifa kufuatia kuuawa kwa ndugu zao hao.

'Leo tumewapoteza Myuran na Andrew. Watoto wetu, kaka zetu, ' walisema katika taarifa hiyo.

'Miaka kumi tangu walipokamatwa, walifanya kila lililowezekana ili waachiwe, na kuwasaidia wengine, lakini hawakusikilizwa.
Mary Jane Fiesta Veloso (katikati), ambaye kifo chake kiliahirishwa baada ya mwanamke mmoja kujisalimisha nchini Ufilipino, akisema kuwa yeye ndiye aliyemdanganya dada huyo kubeba dawa hizo za kulevya.

Jeshi la Nigeria laokoa wasichana 200 na akina mama 93Kundi la wasichana wa Nigeria waliotekwa na Boko Haram kutoka kijiji cha Chobok mwaka 2014. Bado haijathibitishwa kama wasichana hao waliookolewa ni wale kutoka Chibok.


LAGOS, Nigeria
JESHI la Nigeria limewakomboa wasichana 200 na akina mama 93 ambao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Hilo lilitokea wakati wa zoezi la kijeshi kuurejesha msitu wa Sambisa uliopo kaskazini ya Nigeria kutoka kwa kundi la kijeshi la Kiislamu.

Hatahivyo, ilithibitishwa kuwa watu hao waliookolewa sio wale wasichana wakiwemo wanafunzi 300 Wakristo waliotekwa mwaka jana huko hibok na kundi hilo.

Jeshi liliweka katika ukurasa wao wa Twitter taarifa ikisema: 'Jeshi mchana huu iliwaokoa wasichana 200 na akina mama 93 kutoka msitu wa Sambisa. 

'Hatuwezi kuthibitisha kama wasichana wa Chibok wamo katika kundi hili la watu walookolewa,' ilisema taarifa hiyo, ikiongeza kuwa jeshi la Nigeria pia limeharibu kambi tatu zinazoendeshwa na askari hao wa Boko Haram.

Baada ya kutekwa na Boko Haram, baadhi ya wasichana walionekana katika picha wakiwa wamevalishwa mavazi marefu ya hijab.
Wanadiplomasia na wapigania haki za binadamu wamesema kuwa wanaamini kuwa wasichana hao walikuwa wakishikiliwa msituni umbali wa karibu maili 60 kutoka Chibok.

Jeshi la Nigeria likisaidiwa na ndege za kivita lilivamia msimu huo ambao ni eneo la zamani la msimu wa hifadhi la kikoloni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni sehemu ya zoezi la kutaka kulipokonya jimbo hilo kutoka kwa Boko Haram.

Kanali Sani Usman alisema: 'Jeshi liliokoa wasichana 200 na wanawake 93.

'Hatahivyo, sio wale kutoka Chibok, kijiji ambacho zaidi ya wasichana 200 walitekwa Aprili mwaka 2014.

'Hadi sasa, (jeshi) limeharibu na kufagia kabisa Sassa, Tokumbere na kambi zingine mbili katika eneo la Alafa, zote zikiwa katika msitu wa Sambisa.

Taarifa hiyo ilisema kuwa wasichana na akina mama hao watafanyiwa vipimo vya afya ili kujua kama walitekwa nyara au kuolewa na askari hao wa Boko Haramu.

'Kesho pia watahojiwa kujua kama walikuwa ni wake wa askari wa Boko Haram, kama wanatoka Chibok, au wako kwa muda gani katika kambi, na kama wana watoto.

Boko Haram waliteka wanafunzi wakike 200 karibu na kijiji cha Chibok Aprili mwaka jana, ambapo jumuiya ya kimataifa imelaani kitendo hicho.

Wanafunzi hao walichukuliwa katika malori usiku wa Aprili ya tarehe 14 na 15, abaada ya magaidi kutoka Boko Haram-wakidai kuwa elimu ya Magharibu ni dhambi-na walivunja shule kwa kujidai kuwa wao ni walinzi.

Wanafunzi hao walilazimishwa kubadili dini na kuwa Waislamu na kuolewa na wanajeshi wa kundi hilo.

Dunia nzima ililaani uvamizi huo na kufanya kampeni kubwa inayojulikana kama '#bringbackourgirls' lakini zaidi ya 200 bado hawajapatikana huku wengine wakidhaniwa kuwa waliachiwa au kuuawa.

Wiki iliyopi Nigeria niliadhimisha mwaka mmoja tangu kupotea kwa wasichana hao huku rais mpya wan chi hiyo Muhammadu Buhari, aliyeshinda uchaguzi wa urais wiki mbili zilizopita, alisema kuwa watafanya kila njia kuhakikisha wasichana hao wanarejeshwa nyumbani.

'Serikali yangu itafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani wasichana hao, aliongeza rais huyo.

Monday, 27 April 2015

Hakuna wa kuizuia Yanga kutwaa ubingwa leo


Kikosi cha Yanga.

Na Seba Nyanga
HAKUNA wa kuizuia Yanga leo kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 25 wakati itakapocheza na Polisi Morogoro katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa leo tunaweza kuufananisha na ule usemi wa sungura kumkaba tembo, kwani Yanga katika ligi hiyo ni sawa na tembo wakati Polisi Moro inafananishwa na sungura kutokana na uwezo na udogo wake.

Kwa sababu ya kutokuwepo wa kuizuia Yanga ndio maana tayari wanachama, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wameandaa sherehe na kutoa ratiba kamili ya kusheherekea ubingwa huo.

Kimsimamo; Yanga ambayo ni bingwa wa kihistoria wa Tanzania na iliyopo kileleni ikiwa na pointi 52, inahitaji pointi tatu tu ili iweze kuwa bingwa kamili wa msimu wa 2014/15 na kujikatia tiketi ya kuliwakilisha taifa katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Ikiifunga Polisi Moro leo itakuwa imefikisha jumla ya pointi 55, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kati ya 13 zinazoshiriki ligi hiyo inayoshirikisha timu 14.

Azam inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 inaweza kufikisha pointi 54 tu tena endapo itafanikiwa kushinda mechi zake zote zilizobaki.
 
Ni kweli katika soka lolote linaweza kutokea, lakini ukilinganisha uwezo wa Yanga, hivyo leo kama Polisi Moro itaifunga timu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, basi ni sawa na mende kuangusha kabati, kitu ambacho ni ngumu kutokea.

Katika mchezo wao wa kwanza, Yanga iliibamiza Polisi Moro kwa mabao 5-0 katika mzunguko wa kwanza, hivyo ni dhahiri kuwa timu hiyo haina ubavu kuzuia makali ya Yanga.

Taarifa za Yanga zilisema kuwa uongozi wa klabu hiyo tayari umeanza maandalizi kusherehekea ubingwa kwa mtindo wa aina yake.

Uongozi wa Yanga unapenda kuwaalika wanachi wa Tanzania na nchi jirani kuungana nasi leo Jumatatu katika shamra shamra za ushindi wa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Sisi kama Yanga tumejipanga kwa staili ya tofauti kabisa katika kuuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, iliongeza taarifa hiyo.

Naye kocha Hans van der Pluijm alisema anatarajia timu yake kutwaa ubingwa leo.

Yanga watasafiri kwenye Tunisia kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho na Etoile de Sahel ya huko itakayochezwa mwishoni mwa wiki hii.