Saturday, 21 March 2015

Wanariadha kibao kushiriki mbio za dunia za nyikaMONACO, Ufaransa
ZIMEBAKI siku chache kabla ya kufanyika kwa mbio za dunia za nyika zitakazofanyika Guiyang, China Machi 28, mashindano ya mwaka huu yatashindanisha wanariadha wengi zaidi.

Zaidi ya wanariadha 447 kutoka nchi 51 wanajiandaa kutua Guiyang kwa ajili ya mbio hizo ikiwa ni idadi zaidi ya wale walioshiriki mwaka 2013 (wanariadha 400 kutoka nchi 41), 2011 (wanariadha 423 kutoka nchi 51) na 2010 (wanariadha 437 kutoka nchi 51).

Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) wiki ijayo litachapisha orodha, lakini hapa tunaangalia wanariadha 10 ambao watakuwa tishio katika mbio hizo.

Wakubwa wanaume:

Bedan Karoki (KEN)

Bingwa huyo wa Kenya anachukuliwa zaidi kama mmoja wa wanariadha mahiri katika mbio za nyika duniani, lakini Karoki ameshinda mara mbili mbio hizo. 

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 atashiriki mbio za dunia za nyika zitakazofanyika Guiyang.

Polat Kemboi Arikan (Uturuki)
Arikan alitawala mbio za nyika za Ulaya Desemba, lakini katika mbio za Guiyan anatarajia kuwa mmoja wa washindani wakubwa kwa sasa katika mbio hizo.

Chris Derrick (Marekani)
Mshindi wa timu iliyotwaa medali ya fedha miaka miwili iliyopita, Derrick ndiye tegemeo la Marekani huko China.

Badaa ya kushinda mbio za kilometa nane huko Edinburgh Januari, aliendelea kushinda mbio za taifa za nyika kwa sekunde 30.

Wanawake wakubwa
Emily Chebet (Kenya)
Bingwa mara mbili wa mbio za nyika za dunia na aliongezwa katika timu ya taifa ya Kenya.

Ding Changqin (China)
Bingwa wa medali mbili katika mbio za uwanjani mwaka jana katika mashindano ya Asia, Ding anabeba matumaini ya taifa.

Mwaka jana alishinda mbio fupi na ndefu katika mashindano ya mbio za nyika ya China kwa tofauti kubwa.

Jacqueline Martin (Hispania)
Ni mwanariadha mwenye umri wa miaka 40 na atashiriki mashindano hayo kwa mara ya 14, ikiwa ni miaka 23 tangu aanze kushiriki mbio hizo. Ni wanawake wawili pekee katika historia ya mashindano hayo wenye uzoefu zaidi ya wanariadha wengine.

No comments:

Post a Comment