Sunday, 1 March 2015

Guinea yapinga Afcon kuchezwa Juni 2023




CONAKRY, Guinea
WENYEJI wamefunguka na kusema kuwa hawakubaliani na fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2023 kuchezwa mwezi Juni ili kuziwezesha fainali za Kombe la Dunia kufanyika Qatar, alisema waziri wao wa michezo.
Domani Dore alipingana na taarifa ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) Jerome Valcke, ambaye wiki iliyopita alisema kuwa, fainali za Mataifa ya Afrika 2023 zinatakuwa kusogezwa mbele kwa miezi sita hadi Juni kutoka katika muda wake wa kawaida wa mwezi Januari.
Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zimepangwa kufanyika Novemba na Desemba, kufuatia mapendekezo ya kamati ya maandalizi.
Valcke alisema kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwezi mmoja baadae ni jambo lisilowezekana, na aliongeza kuwa anakubaliana na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuhamisha fainali hizo zinazoshirikisha jumla ya timu 16 baadae mwaka huo.
Hatahivyo, Guinea, imesema kuwa itapinga tarehe hizo mpya.
"hatuwezi kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwezi Juni, ni kipindi cha mvua, “’alisema Dore alipozungunza na televisheni ya Guinea.
"Caf walitakiwa kusikiliza ushauri wa Guinea kuwa kama sisi ni taifa tunatakiwa kuamua tarehe gani zifanyike. Tunaelewa matatizo yanayolizunguka Kombe la dunia na kugongana na fainali za Mataifa ya Afrika.
"Lakini Caf walitakiwa kusikilisha maoni yetu. Mwezi juni , haiwezekani, " aliongeza Dore.
Shirikisho hilo la Soka la Afrika limesisitiza kuhusu fainali Mataifa ya Afrika 2023 nchini Guinea, likisema kuwa "uamuzi kuhusu Afcon 2023 utatolewa na Kamati ya Utendaji ya CAF, na sio mtu mwingine, wakati utakapofika."

No comments:

Post a Comment