Tuesday 29 December 2015

Sare na Chelsea yampa kiburi Van Gaal na kusema kamwe hatojiuzulu ng'oo



Kocha Mkuu wa Man United, Louis van Gaal (kushotot) akiangalia timu yake ikitoka suluhu na Chelsea pamoja na msaidizi wake, yan Giggs.

LONDON, England
KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal anasema kuwa kamwe hatajiuzulu licha ya kushuhudia timu yake ikiteleza hadi nje ya nne bora katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Suluhu ya Jumatatu nyumbani dhidi ya helsea ina maana kuwa, Man United sasa imeshindwa kuibuka na ushindi katika mechi nane katika mashindano yote.

Hiyo haijawahi kuwatokea tangu mwaka 1990 na kuiacha klabu hiyo ikiwa pointi tano nyuma ya wapinzani wao wa jiji Manchester City ambao wako katika nafasi ya nne katika msimamo huo.

Lakini bado Van Gaal alikuwa na moyo na kusema: "Wakati wachezaji wanaonesha kiwango kama kile pamoja na shinikiza kibao, kwa kweli hakuna sababu ya kuachia ngazi.

'Wachezaji wako Tayari Kupambana'
Siku chache zilizopita kocha, ambaye alianza kuifundisha Man United tangu Julai mwaka jana, alikuwa majaribuni.

Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 64 aliibuka kabla ya Krismas baada ya vyomo vua habari kukosoa nafasi yake.

Baadae timu yake ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Stoke, kipigo kilichoongeza shinikizo la kutimuliwa huku ikidaiwa kuwa nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Jose Mourinho, aliyetimuliwa na Chelsea Desemba 17.

Kabla ya mchezo huo wa Jumatatu dhidi ya the Blues, baadhi ya mashabiki walikuwa wamebeba skafu zenye jina la Mourinho, ambazo zilikuwa zinauzwa nje ya Uwanja wa Old Trafford.

Mabingwa Simba kuanza kampeni dhidi ya Jamhuri Kombe la Mapinduzi ZNZ




Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga na washindi wa pili Azam FC wako katika kundi moja la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na waandaaji wake.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumamosi, Januari 2 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa Kamati ya Michuano hiyo, jumla ya jumla ya timu nane zinatarajia kushiriki na zumepangwa katika makundi mawili, huku mabingwa watetezi Simba wakipangwa kufungua dimba na Jamhuri ya Pemba.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa, kabla ya mchezo huo wa  ufunguzi, jioni kutakuwa na mchezo utakaozikutanisha timu za Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) dhidi ya Watoza Ushuru wa Uganda (URA).

Simba katika mchezo huo imepangwa katika Kundi A pamoja na timu za JKU, URA na Jamhuri.

Kwa upande wa mahasimu wao Yanga, wenyewe wako katika Kundi B pamoja na timu za Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro, Azam FC na Mafunzo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Sharifa Khamis ametaja viingilio vya michezo hiyo kuwa ni  Sh. 10,000,5,000, 3000 wakati Urusi ni Sh. 2,000 tu.

Simba walitwaa taji hilo mwaka jana kwenye Uwanja wa Amaan baada ya kuichapa Azam FC.
 

Monday 28 December 2015

Jose Mourinho anasubiri kibarua Manchester United kabla hajarudi Real Madrid



LONDON, England
KOCHA Jose Mourinho anajaribu kuzuia vishawishi vya kurejea haraka katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid wakati akisikilizia hali inavyoendelea katika klabu ya Manchester United na kwingineko Ulaya kabla hajafanya maamuzi ya mwisho kuhusu kibarua chake kijacho.

Madrid, ambako Mourinho aliondoka mwaka 2013 na kurudi Chelsea, wameonesha nia ya kumrejesha kocha wao huyo wazamani kuchukua nafasi ya mpinzani wake wazamani Rafa Benitez.
Lakini Mourinho kwa sasa anaonekana kama hana mpango wa kurejea Madrid.

Pia familia ya Mourinho, mkewe Tami, mtoto wake wa kike Matilde na yule wa kiume Jose junior hawana hamu ya kurejea katika jiji hilo la Hispania,ambalo walikaa kwa zaidi ya mismu mitatu.

Kingine kinachomfanya kocha huyo Mreno kutokuwa na hamu ya kurejea Madrid ni ile hali ya kutoelewana na baadhi ya wachezaji lakini tangu atimuliwe na Chelsea, amekuwa katika mipango ta Madrid.

Kwa sasa iko katika nafasi ya tatu, ambapo Jumatano watacheza na Real Sociedad na Valencia ya Gary Neville wayakwaana nayo Jumapili kabla ya kuanza kwa mapumziko ya majira ya baridi.

Timu hiyo ilifunga mabao 10 walipocheza dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga, na kufuatia na kipigo kutoka kwa Villarreal.

Kwa sasa, Mourinho anasubiri kuangalia mwenendo wa rafiki yake na bosi wake wazamani Louis van Gaal Man United, ambao leo waikabili Chelsea kwenye Uwanja wa Old Trafford. 

Kocha huyo Mreno alitumia wiki kadhaa zilizopita akivua samaki na marafiki zake katika pwani jirani na Setubal. Sasa amekwenda Ureno kwa ajili ya mapumziko na familia yake.

Mohamed Elneny: Arsenal yafanya mazungumzo kutaka kumsajili kiungo huyo wa Basel



LONDON, England
KLABU ya Arsenal iko katika mazungumzo na FC Basel kuhusu kumsajili kiungo wa kati Mohamed Elneny (pichani).

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Uswisi mwaka 2013 na ametwaa mataji ya ligi katika kila msimu alioichezea timu hiyo.

Kiasi cha ada kilichoelezwa ni kama pauni milioni 5 na Elneny anahitaji kibali cha kufanyia kazi ili kuichezea timu hiyo.

Mchezajji huyo ruksa kuichezea Arsenal katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya Basel kushindwa kufuzu mwaka huu katika hatua ya makundi.

Elneny alikuwemo katika kikosi cha Basel kilichoibuka na ushindi dhidi ya Chelsea katika mashindano ya msimu wa mwaka 2013-14.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger yuko mbioni kuimarisha kikosi chake hasa katika nafasi ya kiungo wa kati baada ya Francis Coquelin na Santi Cazorla kupata majeraha makubwa, huku Aaron Ramsey na Mikel Arteta nao pia wako nje ya uwanja na Jack Wilshere bado hajarejea uwanjani.

Hatahivyo, Elneny anaonekana kama sehemu ya mpango ya muda mrefu wa Wenger na sio kuziba pengo, wakati atakapojiunga na klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini ya London.

Wilshere atakuwa nje ya uwanja angalau hadi mwezi Februari.
Kocha huyo wa the Gunners alikiri kuwa, hana uhakika kama Wilshere atarejea haraka uwanjani, lakini sio kabla ya Februari.

Kiungo huyo wa England alitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa angalau miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji Septemba baada ya kuumia katika mguu wa kulia, lakini makadilio hayo yameongezeka.

"Nilisema Februari lakini ukweli sina uhakika, alisema Wenger wakati timu yake ilipochezea kichapo cha mabao 4-0 katika Ligi Kuu ya England kutoka kwa Southampton huku leo Jumatatu timu hiyo ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Bournemouth.

Kibira aendelea na matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili




Mwenyekiti wa Chaneta, Annie Kibira (kulia) na mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi wakati wa kukabidhi bendera ya taifa timu ya taifa ya netiboli iliyodhiriki mashindano ya Afrika nchini Namibia mwaka huu. Timu hiyo haikufanya vizuri.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Annie Kibira anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupooza.

Kibira alianguka ghafla baada ya kupatwa na shinikizo la damu na kuanguka wakati akisimamia mashindano ya netiboli ya Muungano kisiwani Zanzibar na baadae kulazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo kabla ya kuhamishiwa Muhimbili.

Mashindano ya Muungano ya netiboli yalimalizika wiki iliyopita kwenye Uwana wa Gymkhana huku mabingwa wa Tanzania Bara Uhamiaji wakiibuka mashujaa baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

Mtoto wa Kibira, Kelvin amesema kuwa mama yake kesho Jumanne anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya MR1 katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu zaidi.

Alisema kuwa Kibira amelazwa Mwaisela word namba 7 chumba namba 311, ambako anaendelea na matibabu baada ya kupooza upande wa kulia kuanzia mguuni hadi usoni.

Alisema kuwa kutokana na kuongozana kwa Siku Kuu za Maulidi, Krismas na wikiendi, ndiko kulikosababisha mama yake kuchelewa kufanyiwa baadhi ya vipimo.

Alisema kuwa leo Jumatatu mama alitarajia kuanza kufanyiwa mazoezi ikiwa ni sehemu ya matibabu yake.
Akizungumzia hali ya mama yake, Kelvin alisema kuwa anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa awali.

Kibira kabla ya mashindano hayo ya netiboli ya Muungano alihudhuria Mkutano Mkuu wa kawaida wa mwaka wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) mjini Zanzibar, kabla ya kufanyika mashindano hayo ya Muungano, huku akiwa mwenye afya tele.