![]() |
Nemanja Matic wa Chelsea akimuangusha chini Saido Mane na kuipatia Southampton penati iliyosawazisha bao na kuzifanya timu hizo kutoka sare 1-1. |
LONDON, England
KOCHA wa Chelsea Jose Mourinho anadai kuwa Arsenal imerejea
katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya England baada ya Chelsea kukaliwa
kooni na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Southampton.
Arsenal iliibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 dhidi ya West
Ham Jumamosi na kikosi hicho cha kocha Arsene Wenger, ambacho hakijashinda taji
hilo tangu mwaka 2004, sasa kiko nyuma ya Chelsea kwa pointi saba tu.
Mabingwa wa England Manchester City wenyewe walijikuta
wakipunguzwa kasi ya kutetea taji hilo baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 na Burnley
huku Chelsea ikitoka sare kwenye uwanja wake wa Stamford Bridge.
Mourinho alisema: ‘Bila shaka Arsenal wako katika mbio hizo. Wako pointi
saba nyuma ya Chelsea, lakini ina mechi moja pungufu ya kucheza.
‘Timu zote City na Arsenal wako katika mbio
za kuwania ubingwa. Itategemea hali ya Arsenal kwa sasa-kipigo cha bao 3-1
kutoka kwa Monaco au kipigo cha 3-0 dhidi ya West Ham?
Mourinho anaamini kuwa penati ya jana ilitolewa
kimakosa na kuinyima kuwa point inane mbele ya Manchester City kileleni mwa
msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Kocha huyo Mreno alipigwa faini ya pauni Milioni 25,000
kwa kitendo chake cha kusema kuwa 'kuna kampeni ya wazi'dhidi ya timu yake
baada ya Cesc Fabregas kunyimwa penati na badala yake kupewa kadi kwa madai ya
kujirusha katika sareya Desemba 28 kwenye uwanja wa St Mary's.
No comments:
Post a Comment