Thursday, 12 March 2015

Cole alimwa faini kwa kuwakashfu mashabiki mtandaoniLONDON,England
MSHAMBULIAJI wa West Ham Carlton Cole (pichani),amelimwa faini ya pauni 20,000 na Chama cha Soka kwa kutoa maneno ya kashfa kwa mashabiki wa Tottenham katika mtandao wa Twitter.

Cole, mwenye umri wa miaka 31, pia amepewa onyo kali kuhusu na kutotakiwa kufanya kosa hilo tena.

Awali mchezaji huyo alikiri kuvunja sheria za chama hicho cha soka kuhusu wachezaji kutumia mitandao ya kijamii.

Mchezaji huyo wazamani wa kimataifa wa England aliandika maneno ya kejeli akiwajibu mashabiki kufuatia sare ya mwezi uliiopita ya 2-2 kati ya Hammers na wapinzani wao wa jiji la London wa Spurs.

Aprili mwaka 2011, Cole alipigwa faini ya pauni 20,000 kwa kutoa maoni yake katika Twitter wakati England ikiceza na Ghana mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu.

Cole ameichezea Hammers mechi 17 msimu huu na amefunga mabao matatu.

No comments:

Post a Comment