MADRID, Hispania
NYOTA wazamani wa Barcelona anaamini kuwa endapo
mmoja kati ya nyota hawa wawili wa La Liga ataondoka katika klabu yake ya sasa,
hakuna shaka kuwa itapungusa sana ushindani wao.
Mshambuliaji wazamani wa Barcelona Patrick Kluivert (pichani), anaamini
kuwa ni muhimu kwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuendelea kubaki Hispania
ili kuweka hai upinzani wao.
Wawili hao wanacheza timu tofauti za Barca na Real
Madrid zinazoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga tangu Ronaldo ajiunge mwaka
2009, huku Messi akiwa Camp Nou tangu mchezaji huyo aanze kuichezea kwa mara ya
kwanza timu hiyo miaka mitano kabla.
Wawili hao ndio wamekuwa wakitaweala tuzo za mchezaji
bora wa dunia au Ballon d'Or kwa miaka saba mfululizo, huku Messi akishinda
tuzo hizo mara nne na Mreno Ronaldo akitwaa mara tatu, huku viwango vyao vya
ajabu vikileta malumbano miongoni mwa wapenda soka.
Kluivert,aliyeichezea
Barcelona kwa miaka saba kuanzia mwaka 1998, anafikiri arjen Robben wa Bayern
Munich ndiye mchezaji pekee anayewakaribia wachezaji hao wawili kwa viwango kwa
sasa.
"Wote ni wachezaji wazuri ," alisema kocha
huyo wa Curacao katika mtandao wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa). "Kitu
muhimu sana ni kuwa wote kwa sasa wanacheza soka Hispania. Endapo mmoja
angekuwa Hispania na mwingine England, upinzani ungekuwa tofauti.
"Lakini, acha tuseme ukweli, wachezaji wote ni
bora duniani na baadae ndio anakuja Robben na wengine. Messi ni mchezaji wa
aina yake: mguu wake wa kushoto ni kama dhahabu. Kila anachofanya kinafanana na
dhahabu.
No comments:
Post a Comment