Sunday, 15 March 2015

Mjane amuonesha kadi nyekundu mahakamni muuaji wa mumewei


Mjane wa Bieniewicz,  Kris akimuonesha  kadi nyekundu  Saad baada ya mchezaji huyo kuhumumiwa kwenda jela miaka nane kwa kumuua mume wa mama huyo.MICHIGAN, Marekani
MCHEZAJI soka wa ridhaa ametupwa jela baada ya kumuua mwamuzi kwa kumtwanga ngumi moja bkufuatia kuoneshwa kadi katika mchezo wa ligi ya hapa, imeelezwa.

John Bieniewicz alikuwa mbioni kumuonesha Bassel Saad kadi ya pili ya njano na ingemfanya atoke nje ya uwanjani, ndipo mchezaji huyo mwenye umri wa mkiaka 37 alipomtwanga sumbwi mwamuzi huyo na kutoka nje wakati mwamuzi huyo akipata matibabu pale chini alipoanguka.
 
Mwamuzi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 44, alifariki dunia siku mbili baada ya mchezo huo uliofanyika Detroit juni mwaka jana.
Saad alikubali kosa hilo la kuua bila kukusudia na alihukumiwa kifungo Ijumaa angalau miaka nane jela.

Wakati Saad akikaribua kuondolewa kutoka mahakamni na kupelekwa jela, mjane wa marehemu alionesha kadi nyekundu na kusema: "Napenda kumpa bwana Saad kadi nyekundu ambayo alistahili kupewa. "

Jaji Thomas Cameron alisema: "Kwa wema au ubaya, wewe umedhihirisha kwa watu wengi kuwa ni kosa kufanya vurugu michezoni."

Mahakama ilimuaru Saad kulipa pauni 9,200 (sawa ba dola za Marekani 6,200) kama gharama za mazishi ya mwamuzi huyo.

Watungaji wa sheria wa Michigan wanatakiwa kufikiria makosa mapya kwa wanaoumiza waamuzi wa michezo.

Mjane huyo alisema kifungo cha miaka nane alichohukumiwa mchezani huyo hakilingani na thamani ya utu wa mumewe.

Mama huyo ambaye ni kocha wa timu ya mpira wa kikapu, alisema kuwa tangu mumewe afariki dunia, yeye na watoto wake wawili wamekuwa wakiishi kwa tabu sana.
Bassel Saad akilia mahakamani baada ya kuhukumiwa miaka nane kwa kosa la kumuua mwamuzi katika mchezo wa soka
No comments:

Post a Comment