Tuesday, 17 March 2015

Serena Williams atinga robo fainali kwa mbindeCALIFORNIA, Marekani
SERENA Williams (pichani), baada ya kuanza vibaya ameibuka na kumchapa Mmarekani mwenzake Sloane Stephens na kutinga robo fainali ya mashindano ya tenisi ya BNP Paribas Open huko Indian Wells.

Bingwa huyo namba moja, mwenye umri wa miaka 33, alipoteza seti ya kwanza lakini alipigana na kushinda mchezo huo kwa 6-7 (7-3) 6-2 6-2.

"Bado ninajaribu kuangalia kufanya vizuri, " alisema Williams. 

Williams alikuwa akicheza mchezo wake watatu kwenye uwanja wa California baada ya kumaliza miaka 14 ya kugomea mashindano hayo.

Mdada huyo aligoma kucheza mashindano hayo baada ya kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi mwaka 2001.

No comments:

Post a Comment