Monday, 16 March 2015

Serena Williams atinga 16 bora Indian Wells


CALIFORNIA, Marekani
BINGWA namba moja katika mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa akina dada Serena Williams (pichani), ametinga hatua ya 16 bora katika mashindano ya Indian Wells baada ya kuibuka na ushindi wa 6-2 6-0 dhidi ya Zarina Diyas wa Kazakhstan.

Kwa ushindi huo, Williams sasa atakutana na Mmarekani mwenzake Sloane Stephens baada ya dakika 53 za raundi ya tatu ya mchezo wa mashindano ya BNP Paribas Open.

Williams, ambaye aligomea kushiriki mashindano hayo kwa miaka 14 baada ya kuzomewa mwaka 2001, anasema sasa anajisikia vizuri kucheza katika mashindano hayo ya California.

"Sasa najisikia kurejea katika hali yangu ya kwaida hapa," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

"Niliweza kupumzika kwa sababu niliweza kufanya mengi kwa usahihi na sikufanya makosa mengi kama nilivyofanya katika mchezo wangu wa raundi iliyopita,"

Stephens beat alimfunga bingwa mara mbili Svetlana Kuznetsova 7-6 (7-4) 1-6 6-4 na kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ambayo atakutana na Williams.

Kwa upande wa wanaume, Mswisi Roger Federer alimchakaza Diego Schwartzman 6-4 6-2 katika raundi ya pili ya mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment