Thursday 19 March 2015

Micho amtema Emmanuel Okwi The Cranes


Mganda Emmanuel Okwi akishangilia moja ya mabao yake aliyofunga katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

KAMPALA, Uganda
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda ya The Cranes, Micho Sredojevic ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa ugenini dhidi ya Nigeria huku Emmanuel Okwi wa Simba akimuweka kando.

Okwi anayeichezea Simba ya Tanzania kwa sasa yuko katika kiwango cha juu baada ya kuifungia timu yake bao pekee walipoichapa Yanga 1-0 kabla ya kufunga dhidi ya Mtibwa.
Wakati Micho akimuacha Okwi, wachezaji wengine wanaocheza soka Tanzania wameitwa akiwemo  Brian Majwega wa Azam FC na Jjuko Murushid wa Simba.

The Cranes itaikabili Super Eagles Jumatano ya wiki ijayo huko Akwa Ibom katika moja ya mechi kibao zitakazochezwa katika kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wiki ijayo.

Kikosi kina makipa wanne, mabeki nane, viungo tisa na washambuliaji wanne.

Kipa Dennis Onyango, beki Isaac Isinde, kiungo Kizito Luwagga na mshambuliaji Geoffrey Massa ni miongoni mwa baadhi ya wachezaji wenye uzoefu walioitwa katika kikosi hicho cha Micho, ambao wote walikuwemo katika kikosi kilichoshindwa kufuzu kwa Mataifa ya Afrika 2015.

Beki Savio Kabugo hayumo kutokana na maumivu wakati nahodha Andy Mwesigwa ataukosa mchezo huo.

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi naye pia hayumo katika kikosi licha ya mchezaji huyo kuonesha makali yake katika kikosi cha Simba hivi karibuni walipocheza dhidi ya Yanga.

Kwa mara ya mwisho Uganfa na Nigeria zilikutana mwaka 2007 katika mechi za kufuzu kwa fainali za Kombela Mataifa ya Afrika za 2008 huku Uganda ikiondoka na ushindi wa 2-1 katika mchezo uliofanyika Kampala na kufungwa 1-0 na Super Eagles ugenini huko Abeokuta.

Makipa: Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns-Afrika Kusini), Robert Odongkara, (St. George FC-Ethiopia), Jamal Salim (El Merreikh-Sudan), Ismail Watenga (Vipers FC Uganda)

Mabeki: Isaac Isinde (St. George- Ethiopia), Jjuko Murushid (Simba SC-Tanzania), Richard Kasagga (Salam Zgharta-Lebanon), Joseph Nsubuga (Bright Stars Uganda), Ibrahim Kiyemba (Lweza FC-Uganda), Bakaki Shafiq (Express FC-Uganda), Alex Kakuba (Estoril Praia-Portugal) na Godfrey Walusimbi (Gor Mahia- Kenya)

Viungo: Dennis Guma (Al Ahed- Lebanon), Khalid Aucho (Gor Mahia -Kenya), Kizito Keziron (Vipers FC-Uganda), Derrick Tekwo (Kira Young), Mike Azira (Seattle Sounders-Marekani), Chrizestom Ntambi (SC Villa-Uganda), Brian Majwega (Azam FC- Tanzania), Kizito Luwagga (Sporting Covilha Ureno) na  Farouk Miya (Vipers FC- Uganda)

Washambuliaji: Geoffrey Massa (Pretoria University Afrika Kusini), Brian Umony (Saint George FC-Ethiopia), Robert Ssentongo (URA FC-Uganda) na Patrick Edema (Beira Mar-Ureno)

No comments:

Post a Comment