Tuesday, 3 March 2015

Wawili kushiriki mashindano ya vijana Ethiopia Mwanariadha wa shule ya Filbert Bayi Rose Seif akishiriki mashindano ya taifa.
 *************
Na Mwandishi Wetu
WANARIADHA wawili na kocha mmoja wameondoka nchini kwenda Addis Ababa Ethiopia kushiriki mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya umri wa miaka 19 yatakayofanyika nchini humo.
Kocha wa timu hiyo Zacharia Gwandu alisdema kabla ya kuondoka kuwa wachezaji hao Rose Seif na Gabriel Gerald watashiriki mbio za mita 5,000 kwa wanawake na wanaume.
Gwandu alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika kuanzia Alhamisi na yatamalizika Machi 8.
Timu hiyo iliondoka kwa ndege ya Kenya Airways na tayari imeshafika Ethiopia kwa ajili ya mashindano hayo.
Aidha, timu hiyo inatarajia kurejea Machi 19 mwaka huu kwa ndege hiyo hiyo ya Kenya.
Gwandu alisema kuwa, wachezaji hao ambao wanasoma katika shule za Filbert Bayi na Winning Spirit za Kibaha na Arusha, walikuwa wakifanya mazoezi chini ya makocha wao.
Gwandu ni kocha wa riadha wa shule ya Filbert Bayi.

No comments:

Post a Comment