Monday, 23 March 2015

Rafael Nadal ajifua kwa mashindano ya WimbledonLONDON, England
BINGWA namba tatu kwa ubora katika mchezo wa tenisi duniani Rafael Nadal atashiriki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011 mashindano ya Aegon.

Mchezaji huyo Mhispania mwenye umri wa miaka 28 huko nyuma alikjiweka fiti kwa ajili ya mashindano ya Wimbledon kwa kucheza michunao ya Halle Open huko Ujerumani mwaka 2012 na 2014.

Lakini Nadal alishindwa kusongambele kuvuka raundi ya nne katika mashindano ya Wimbledon wakati huo na anasema kuwa ndio sababu kubwa iliyomfanya sasa kurejea katika mashindano hayo ya Queen yatakayofanyika Juni.

"Nataka kujaribu tena maswhindano ya Queen ambako angalau viwanja vya nyasi vinafanana na vile vya Wimbledon," alisema.

Nadal alitwaa taji la mashindano ya Aegon mwaka 2008 wakati akielekea kutwaa taji lake moja kati ya mawili ya Wimbledon.

"Nimefurahi sana kurudi, " aliongeza. "Queen ni shindano kubwa, wakati wote nafurahia kucheza.

No comments:

Post a Comment