Monday, 31 July 2017

Kumekucha maandalizi Bagamoyo Marathon 2017

Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mbio za nne za Kihistoria za Bagamoyo zitakazofanyika Jumapili, Agosti 6, mjini humo, yamepamba moto.

Mratibu wa mbio hizo, Dominic Mosha alisema jana kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wanatarajia zaidi ya wanariadha 500 kushiriki mbio hizo mwaka huu.

Alisema mbali na mbio kuu za kilometa 21, pia kutakuwa na mbio za kilometa 10 na zile za kujifurahisha za kilometa tano ambazo hazina zawadi lakini kila mshiriki atapata fulana.

Alisema washindi watatu wa kwanza wa mbio za kilometa 10 kila mmoja ataondoka na medali.

Alisema mbio za mwaka huu zitakuwa na msisimko wa aina yake na zitaandaliwa kwa ubora zaidi, kwani kila mwaka wanapata uzoefu zaidi wa kuandaa kitu bora.

Mosha aliwataka washiriki kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo, ambazo ni maalum kwa ajili ya kutangaza mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

Alisema kuanzia leo wanatarajia kuweka vituo vya usajili wa shiriki ili kuwawezesha wengine ambao hawajaweza kujisajili katika mtandao kufanya hivyo.
Mbio hizo hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na 4Bell, ambapo lengo ni kuibua na kuendeleza vipaji pamoja na utalii mjini Bagamoyo na vitongoji vyake.

Mwaka jana mbio hizo zilifanyika Julai 24 na kushirikisha washiriki kibao kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.


Timu ya Taifa ya Riadha yaagwa, waahidi medali

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimkabidhi bendera ya taifa nahodha wa timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya dunia London, Uingereza, Felix Simbu leo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Saalm. Kulia ni Rais wa RT, Anthony Mtaka na kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Multichoice, Maharage chande.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia yanayoanza wiki hii London, Uingereza imeagwa leo kwa  kukabidhiwa bendera ya taifa jijini Dar es Salaam ikiwa nishara ya kuwa wawakilishi maalum wa nchi yetu katika mashindano hayo makubwa.

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliyekabidhi bendera kwa nahodha wa timu hiyo, Felix Simbu.
Timu hiyo itaondoka afajiri ya kuamkia kesho ikiwa na wachezaji nane, makocha wawili na viongozi wawili, huku Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday akitangulia kuhudhuria vikao mbalimbali akimwakilisha Rais wa RT Anthon Mtaka.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa wizara yake iko bega kwa began a wadau wa michezo haa nchini kuhakikisha kuwa kuwa tunaiga hatua katika sekta hiyo na kuifanya kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa wanamichezo wetu.
Amesema Serikali imejizatiti kikamili katika kuratibu na kurasimilisha michezo haa nchini ili wanamichezo watambue kuwa hiyo ni kazi tena ya heshima kubwa na yenye malio makubwa.

Waziri Mwakyembe ia alionesha kuridhika na viwango vya wachezaji na  kueleza imani yake kubwa kuwa wataweza kutuletea medali.
Waziri ameioneza Kamuni ya Multichoice-Tanzania kwa udhamini wake mkubwa katika maandali ya timu hiyo, ambao kamuni hiyo ilikuwa mdau mkubwa kufanikisha mafunzo katika kambi hiyo.

Naye Rais wa Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, amesema mbali na jitihada kubwa zinazofanywa na chama hicho, bado zipo changamoto nyingi, ambazo zinahitaji nguvu za pamoja ili kuhakikisha kuwa riadha inasonga mbele.
Kwa uande wake Mkurugenzi wa Multichoice, Maharage Chande amesema kuwa kampuni yake ina dhamira endelevu ya kuinua na kuibua vipaji hapa nchini  na ndiyo maana wakaamua kusaidia katika maandalizi ya timu.

Akizungumza baada ya timu hiyo kukabidhiwa bendera, mmoja wa wanariadha hao, Simbu alisema kuwa wao wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanarudi nchini na medali baada ya wanariadha wa Tanzaniua kusindwa kuipata kwa zaidi ya miaka 10.
Kwa mara ya mwisho Tanzania ilitwaa media kutoka katika mashindano ya dunia mwaka 2005 yaliyofanyikia Helsinki, Finland wakati Christopher Isegwe aliotwaa medali ya fedha.

Mbali na Simbu wanariadha wengine wa marathon waliomo katika timu hiyo ni Saida Makula, Stephano Huche, Magdalena Shauri pamoja na Sarah Ramadhani wakati mbio za meta 5,000 watashiriki akina Gabriel Geay na Emmaniel Giniki huku Failuna Abdul atashiriki mbio za meta 10,000.
 
 

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU WAGENI 16 WALIOlNGIA NCHINI KUPITIA JENGO LA WATU MASHUHURI (VIP LOUNGE)

Tarehe 31/07/2017 ehombo kimoja eha habari kilitoa taarifa za upotoshaji kwamba wageni 16 wenye uraia wa Lebanon, Pakistani na Somalia walinaswa katika Kiwanja eha Ndege eha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) baada ya kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP).

Taarifa sahihi za suala hili ni kwamba Tarehe 30107/2017 abiria wanne (4) Raia wa Taifa la Pakistan waliwasili kwenye Kiwanja eha Ndege eha Kimataifa eha Julius Nyerere (JNlA) na kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP Lounge) ambapo nyaraka zao za safari zilikaguliwa na Maafisa wa Uhamiaji na baadae kuruhusiwa kuingia nehini baada ya kujiridhisha kuwa ni halali.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi.
Abiria hao walikuwa na kibali kinaehowaruhusu kutumia ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) kiliehotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Utaratibu uliopo katika matumizi ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP Lounge) JNIA ni kwamba wageni wote toka nje ya nehi wanaohitaji kutumia ukumbi huo wanalazirnika kuomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Wizara husika inapojiridhisha na vigezo vya waombaji,hutoa vibali hivyo.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inatoa wito kwa vyombo vya habari nehini kuandika habari kwa weledi na kuhusisha pande zote zinazohusishwa katika taarifa zao mbalimbali, iii kuepuka mkanganyiko na upotoshaji kwa jamii kwa jambo husika.

TAA ipo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo chochote cha habari kinachowasiliana nacho kutaka ufafanuzi wajambo fulani, ili waweze kuandika kwa umakini na ufasaha zaidi.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA) \--=1; .BW. SALIM MSANGI

Sunday, 30 July 2017

Waziri Mwakyembe kuiaga timu ya riadha inayokwenda London kwa mashindano ya dunia

Mwanariadha Alphonce Simbu akimaliza mbio za Mumbai Marathon.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuiaga timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya 166 ya Dunia yatakayofanyika jijini London, Uingereza  kuanzia Agosti 4 hadi 13.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mawasiliano wa DStv, Johson Mshana, Mwakyembe atakabidhi bendera hiyo kwa timu hiyo katika hafla itakayofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Timu hiyo ambayo iko chini ya Kocha Mkuu, Zakaria Barie ina wachezaji nane, ambao ni Alphonce Simbu, Stephano Huche na Said Makula ambao watakimbia marathon wakati Gabrie Geay na Emmanuel Giniki watashiriki mbio za meta 5,000 huku Sara Ramadhani na Magdalena Shauri watashiriki marathon kwa upande wa wanawake na Failuna Abdi atashiriki meta 10,000.
Wengine watakaokuweo katika timu hiyo itakayoondoka nchini keshokutwa Jumanne ni pamoja na Francis John, ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo.

Barie akizungumza kutoka Arusha jana  kwa njia ya simu alisema kuwa timu hiyo imejiandaa vizuri na iko tayari kupambana kwa ajili ya kupata medali kutoka katika mashindano hayo, ambayo kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata medali mwaka 2005 kutoka kwa Christopher Isegwe aliyepata medali ya fedha katika maratoni mashindano hayo yalipofanyikia Helsinki, Finland.

Kocha huyo alisema kuwa timu yake haina majeruhi wowote na inaondoka ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo makubwa kabisa ya riadha duniani.
Alphonce Simbu (kushoto) akiwaongoza wenzake katika mazoezi ya timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya dunia baadae mwezi huu.
Naye Simbu alisema kuwa wamejipanga kurudi na medali licha ya ugumu uliopo mbele yao,  kwani wanajua ushindani mkali uliopo mbele yao.

Hafla hiyo imedhaminiwa na DStv, na tayari Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday aliondoka jana kwenda London kuhudhuria vikao vitakavyofanyika mapema kabla ya kuanza kwa mashindano hayo akimwakilisha rais wake, Anthony Mtaka.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe (mwenye kifimbo) atakuwa mgeni rasmi katika kuagwa kwa timu ya taifa ya riadha kesho. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda.
 Aidha, mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake kwani wanariadha bora wawili duniani, Usain Bolt wa Jamaica na Mo Farah wa Uingereza watastaafu rasmi mbio baada ya kushirikiria ubingwa wa dunia kwa muda mrefu,
Hizo zitakuwa mbio za mwisho kwa Bolt katika mashindano ya dunia na Farah naye hatakimbia tena mbio za meta 5,000 na 10,000 au mbio za uwanjani na badala yake atageukia marathon, ambazo ni mbio za kilometa 42.

Tuesday, 25 July 2017

Timu ya Madola iliyotwaa medali kurudi Alhamisi

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Tanzania iliyoshiriki Michezo ya sita ya Jumuiya ya Madola kwa vijana na kutwaa medali ya shaba inatarajia kutua nchini keshokutwa Alhamisi kutoka Nassau, Bahamas.

Mwanariadha Francis Damas alitwaa medali hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika mchezo wa mbio za meta 3,000 kwa kutumia dakika 8.37.51 nyuma ya Mkenya na Mcanada walimaliza katika nafasi ya kwanza na pili.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema jana kuwa, timu hiyo yenye wanariadha wawili na waogeleaji wawili, itatua nchini majira ya mchana kwa ndege ya Emerates.

Kwa medali hiyo, Damas anakuwa Mtanzania wa pili kutwaa medali kutoka katika michezo hiyo baada ya Mary Naali aliyetwaa medali kama hiyo katika michezo ya mwaka 2008 iliyofanyika Pune, India kwa upande wa wanawake.

Tangu wakati huo Tanzania haijawahi kutwaa medali kutoka katika michezo iliyofuata ya mwaka 2011 huko Iron Man, Marekani, ambako hatukushiriki na ile ya Samoa (2015), tulitoka mikono mitupu.

Mbali na kutwaa medali, mwanariadha mwingine wa Tanzania Reginal Mpigachai ambaye alitinga fainali ya mbio za meta 800 licha ya kumaliza katika nafasi ya nane, aliboresha tena muda wake binafsi.
Mpigachai awali katika hatua ya nusu fainali alimaliza watano kwa kutumia dakika 2.11.65 na kuboresha muda waka bora wa awali wa dakika 2.13.51 aliouweka katika mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salam.

Katika fainali za meta 800, Mpigachai alimaliza katika nafasi ya nane, huku akitumia dakika 2.10.57 na kuboresha zaidi muda wake bora.
Sio tu kwa vijana hata kwa wakubwa, Tanzania kwa muda mrefu haijapata kutwaa medali katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, ambapo kwa mara ya mwisho kwa wakubwa ilitwaa mwaka 2006 kutoka kwa Samson Ramadhani na Fabian Joseph waliotwaa medali za dhahabu na fedha katika marathon.

Monday, 24 July 2017

Makampuni yajitokeza kudhamini Kilifm Marathon

Mratibu wa mbio za Kilifm Marathon, Nelson Mrashani akizungumza kuhusu mbio hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI zimezidi kujitokeza kufanikisha mbio za pili za Kilifm Marathon zitakazofanyika Agosti 13 mjini Moshi.

Mratibu wa mbio hizo Nelson Mrashani akizungumza kwa njia ya simu jana alisema maandalizi yanaenda vizuri na wamepata wadhamini.

Mrashani aliwataja wadhamini hao kuwa ni pamoja na Wiva Entertaiment, Mr UK, Maji ya Kilimanjaro, Kampuni ya Coca Cola, Radio Kilfm, Temeck Car Tracking, Tanzania Media Foundation, Finca Bank na Ciascom Tech Engeeniring.

Alisema kuwa tayari usajili wa mbio hizo umeanza, ambapo mwaka huu wanatarajia kupata washiriki zaidi ya 3,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Mbio hizo aitahusisha umbali wa kilometa 21, kilometa tano , ambazo zitawashirikisha wafanyakazi wa taasisi mbalimbali pamoja na watu wazima wakati zile za kilometa 2.5 zitakuwa na watoto wadogo.
Zawadi za washindi zitakuwa za aina tofauti, ambapo washiriki wa kilometa 21 wenye umri wa miaka 45-60 na hadi 100 watapewa zawadi maaluma wakati wakibiaji wakawaida watakuwa na kundi lao.

Pia washindi watatu watatu wa mbio zote watapata fursa ya kwenda kutembelea hifadhi ya Ngorongoro ili kuhamasisha utalii wa ndani kupitia Kituo cha Kilifm Sport Centre.

Mrashani alisema kuwa bado wanakaribisha wadhamini wengine ili kuzidi kuboresha mbio hizo ambazo zitakuwa za aina yake mwaka huu.

Rais Magufuli aagiza ujenzi wa jengo la abiria 500 Kiwanja cha Ndege Tabora uanze mara moja

Rais John Pombe Magufuli akipewa maelezo na Mhandisi wa ukarabati, ujenzi na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Neema Joseph wakati wa uzindizi wa mradi huo mkoani humo. Kushoto kwa rais ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Mwandishi Wetu, Tabora
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk  John Pombe Magufuli ameagiza ujenzi wa mradi wa jengo  la abiria 500 kwenye Kiwanja cha Ndege cha Tabora uanze mara moja.

Rais ametoa kauli hiyo mara baada ya kufungua ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Tabora, ambapo alisema sasa abiria wataongezeka kutokana na kukamilika kwa ujenzi huo, hivyo italazimu jengo kubwa lenye kuchukua abiria 500 kwani la sasa lenye uwezo wa kuchukua abiria 50 halitatosha.
“Ninaimani kubwa kwa ujenzi huu lazima idadi ya abiria itaongezeka zaidi, hivyo kwa hili jengo dogo halitatosheleza abiria watakaoongezeka hivyo, namuagiza Waziri (Makame Mbarawa) kuanza mchakato wa ujenzi wa jengo hilo kubwa, ,” alisisitiza Rais Magufuli.

Amesema kutokana na ukarabati na upanuzi huo sasa kiwanja hicho kitaruhusu kutua kwa ndege kubwa zaidi za ndani na nje ya nchi, na kufanya wakazi wa mkoa wa Tabora kutumia uisafiri wa ndani kwa kwenda Dar es Salaam, Burundi, Kenya, Rwanda na maeneo mengine.
Amesema anarajia ujenzi huo utakamilika mapema zaidi na atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa jengo hilo, ambapo aliwapongeza Wizara pamoja na wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Rais amesema serikali yake inataka maendeleo ya kuwa na viwanja vya ndege vya uhakika, barabara na maji na sio siasa, ambazo hazina tija kwa maisha ya wananchi sasa na baadae.
 “Mimi ni Rais wa Watanzania wote na sio wa CCM pekee na ndio maana ninachochea maendeleo tena ya haraka ambayo yatafanikisha wananchi kuwa na maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuitumia miundombinu katika biashara na maisha yao ya kila siku,” amesema Rais.

Katika hatua nyingine, Rais ametaka barabara ya kutua na kuruka kwa ndege irefushwe zaidi ili kuruhusu ndege kubwa kutua kwa wingi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu mbalimbali ya Kiwanja cha ndege cha Tabora.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amesema sambamba na maboresho hayo ya miundombinu katika kiwanja cha ndege cha Tabora, sasa ujenzi wa jengo jipya la abiria unatarajia kuanza mara moja kwa ufadhili wa fedha za mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji ya Uaya (European Investment Bank-EIB), na litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka.

Pia Mbarawa amesema mradi huu wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Tabora umegharamiwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.

Mbarawa amesema mradi huu umejumuisha barabara za kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio, maegesho ya ndege, taa na mitambo ya kiusalama ya kuongoza ndege wakati wowote na kituo cha umeme.
“Kiwanja sasa kimeongezewa uwezo wa kutoa huduma kwa saa 24, na vilevile maboresho yanayofanyika katika viwanja viwanja vya ndege yanalengo la kuvutia ujaji wa mashirika mengi zaidi ya ndege pamoa na kuongeza uwezo wa kuhudumia ndege nyingi zaidi, na sasa serikali inadhamiria ya kununua ndege nne na jum;a itafanya idadi ya ndege sita,” amesema  Mbarawa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kiwanja cha Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi amesema ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja cha ndege cha Tabora umefanyika kwa awamu tatu, ambapo ni kujenga barabara ya kwanza ya kuruka na kutua kwa ndege kwa kiwango cha lami kwa urefu wa mita 1900 na upana wa mita 30.

Msangi amesema awamu ya pili ilihusisha ujenzi wa barabara ya pili ya kuruka na kutua kwa ndege kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 1260 na upana wa mita 23; maegesho ya ndege yenye uwezo wa kuegesha ndege tatu zenye ukubwa wa ATR 72 au Bombardier dash 8 Q400 kwa wakati mmoja; kujenga kiungio yenye urefu wa mita 250; usimikaji wa taa na mitambo ya kuongezea ndege wakati wa kutua na kuruka.

“Hii awamu ya pili ilihusisha vitu vingi ikiwepo pia ujenzi wa kituo cha kufua umeme na usimikaji wa jenereta lenye kVA 500; ujenzi wa uzio wa usalama wa urefuwa kilometa 2.6 na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua,” amesema Msangi.

Amesema awamu ya tatu itahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka; ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani na eneo la maegesho ya magari, ambapo kwa ujumla utafadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na utagharimu sh  za Kitanzania Bilioni 27.

Sunday, 23 July 2017

Wanariadha waahidi medali mashindano ya dunia

Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya ofisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taif ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya dunia London mwezi ujao.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Balozi Maalum wa DStv na moja ya wanariadha wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia mwaka huu yatakayofanyika mwezi ujao jijini London, Uingereza, Alphonce Simbu, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani wamejiandaa vizuri.

Akizunngumza wakati wa ziara maalum ya Ofisa Mwandamizi wa DStv, Johnson Mshana katika kambi hiyo iliyopo Ilboru Arusha ambapo pia alishuhudia mazoezi ya timu hiyo, Simbu alisema kuwa yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanaleta medali nyumbani katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika mapema mwezi ujao.

 “Tumejiandaa vizuri na tuna matumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi mazito na tuko sawasawa kupambana katika mashindano hayo, ” alisema Simbu.
Naye Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Mshana ambayo alitembelea kambi hiyo na kisha kushuhudia mazoezi alisema kampuni yao imefurahishwa sana na mwenendo wa kambi hiyo pamoja na timu nzima.

 “Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi ya timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii ndiyo sababu iliyotusukuma DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya Taifa itakayokwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania tushuhudie medali zikija nyumbani.”

Alisema baada ya DStv kuanza kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita, wameshuhudia mafanikio makubwa sana, ambayo yamewatia moyo sana kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi timu ili hatimaye iweze kufanya vizuri zaidi na kulikwakilisha vyema taifa kwenye michuano ya kimataifa.
“Tulianza na Simbu, amefanya vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi kwa timu yetu ya Tanzania na tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv ilionesha mubashara Mumbai Marathon tukamuona Simbu akishinda, Tukaonesha Mubashara London Marathon, tukaona Simbu akivunja rekodi yake, na tutaonesha mubashara Mashindano ya Dunia Mwezi Agosti, ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua medali kedekede na kuliletea taifa letu sifa kubwa, ” alisema Mshana kwa kujiamini.

Naye Kocha wa timu hiyo Francis John, alisema kuwa kazi kubwa imefanywa na makocho wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi yao kwenda vizuri.
Alisema wanatarajia kuwa wanariadha hao watafanya vizuri,  kwani hata mmoja wao aliyekuwa na matatizo ya magoti sasa anaendelea vizuri na bila shaka atashiriki vizuri kwenye mashindano hayo.

Alisema  jumla ya wachezaji saba  wakiwemo wanawake watatu na wanaume wanne watashiriki, ambao ni Failuna Abdi  atashiriki mbio za meta  10,000, Gabriel Gerald (meta 5,000), huku Magdalena Krispin, Sarah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba na Alphonce Felix Simbu wenyewe watashiriki mbio za marathon.

Huku Emmanuel Giniki akiongeza idadi ya washiriki kwa timu ya Tanzania baada nay eye juzi kufuzu katika mbio za meta 5,000 baada ya kufanya vizuri katika mbio za kimataifa nchini Ubelgiji.
Giniki alimaliza katika nafasi ya saba kwa kutumia dakika 13:13:24 na kuongeza idadi ya washiriki wa Tanzania kufikia wanariadha nane.
Aidha, timu hiyo ya taifa ya Tanzania inatarajia kukabidhiwa bendera Julai 31 katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam tayari kushiriki mashindano hayo ya dunia yatakayoanza Agosti 3 hadi 15.

Mashindano hayo sio mchezo kwani kwa mara ya mwisho Tanzania iliata medali mwaka 2005 yaliofanyikia Helisinki, Finland wakati Christoher Isegwe alipotwaa medali ya fedha baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika mbio za marathon.

Saturday, 22 July 2017

Kilimanjaro International Airport Marathon yaja


Na Cosmas Mlekani
MBIO kubwa zaidi za marathoni zinatarajia kufanyika Moshi Novemba 19 mwaka huu, ambazo zitajulikana kama Kilimanjaro International Airport  Marathoni, imeelezwa.

Mbali na kutarajia kushirikisha wanariadha wengi tena nyota kutoka ndani nan je ya Tanzania, mbio hizo zitakuwa zinaongoza kwa zawadi kubwa, ambao mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh milioni 7 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika mbio za marathon hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mbio hizo, Amini Kimaro akizungumza leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa mbio hizo, ambazo zinaandaliwa na kudhaminiwa na Kilimanjaro Airports Development Company (Kadco) na kusimamiwa na wataalam wa riadha, Amini Kimaro alisema mbio hizo zitaendeshwa kwa utaalam mkubwa.

Kimaro alisema kuwa mshndi wa pili wa mbio hizo za kilometa 42 ataondoka na kitita cha sh milioni 5 huku watatu atakabidhiwa kitita cha sh milioni 4 wakati mshindi wanne atapewa sh milioni 2.5 huku yule watano atabeba sh milioni 2.

Alisema kuwa zawadi za washindi watazitoa hadi kwa mshindi wa 10, ambaye ataondoka na kitita cha sh 500,000.
Mkurugenzi msaidizi wa mbio, Kunda Ndosi.
Mbio za Kilimanjaro Marathon ndizo awali zilikuwa zikichukuliwa kama mbio kubwa zenye zawadi kubwa, ambazo mshindi wa kwanza wa kilometa 42 anaondoka n ash milioni 4 wakati mshindi wa pili anapata sh milioni 2, watatu sh milioni 1, wanne 900,000, watano 600.000 wakati wa 10 ni sh 200,000.

Kwa upande wa mbio za nusu marathon au kilometa 21, zile za Kilimanjaro International Airort wenyewe mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh milioni 4 wakati Kilimanjaro Marathon wanatoa sh milioni 2 tu.
Mbio za Kilimanjaro International Airport zitatoa zawadi za fedha taslimu hata kwa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za kilometa tano, mbio za Kilimanjaro Marathon zenyewe hutoa zawadi za saa na vitu vingine vinavyotolewa na wadhamini wa mbio hizo za kilometa tano.

Hakuna ubishi kuwa zawadi za washindi wa mbio hizo ni nono kweli ukilinganisha na zingine zote zinazofanyika hapa nchini katika vipindi tofauti tofauti vya mwaka.

Mbali na ukubwa wa mbio hizo, pia zitakuwa ni za kipekee kwani zitaanzia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kumalizikia katika maeneo hayo hayo.

Mbio hizi zitajumuisha zile za full marathon, yaani kilometa 42, nusu marathon yaani za kilometa 21 na zile za kilometa tano, ambazo wengine wanaziita mbio za kujifurahisha na hazina zawadi.

Hatahivyo, waandaaji wa mbio hizo za kimataifa za Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro, wenyewe watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi watano, ambao watapata sh 500,000, 300,000, 250,000, 225,000 na 200,000.

Kimaro anasema kuwa wameamua kutoa zawadi nono ili kuvuta nyota wengi wa riadha hapa nchini na nje ya mipaka yetu ili kuzifanya ziwe kubwa zaidi.

Anasema kuna viwanja kadhaa vya ndege duniani vimekuwa vikiandaa mbio ili kuvuta watalii na watu wengine kama vile Dubai Marathon na Helsink nchini Finland.
Anasema mshindi wa pili ataondoka na kitita cha sh milioni 5, wakati wa tatu atapewa sh milioni 4,  huku yule wa nne atapewa sh milioni 2.5, watano sh milioni 2 na wa sita sh milioni 1.

Mshindi wa saba ataondoka na sh 800,000 wakati yule wa tisa atapata 700,000 wa tisa na 10 atapata sh 600,000 na 500,000.

MBIO MPYA ZA WANAFUNZI
Hii ni mara ya kwanza kwa waandaaji wa mbio kuwakumbuka wanafunzi, ambapo kutakuwa na mbio maalum za wanafunzi za kilometa 21, ambapo wanafunzi watatumia fedha za ushindi kulipia ada zao.

Mbali na kuwashindanisha wanafunzi, pia mbio hizo za nusu marathoni zitashirikisha wanariadha wa kawaida ambao nao watakuwa na zawadi zao.

Zwaadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao watashindana katika kilometa 21 zikuwa ni sh milioni 4 kwa mshindi wa kwanza wakati mshindi wa pili ataondoka sh milioni 3 wakati mshindi wa tatu atapata milioni 2.5.

Kimaro ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Riadha Wilaya ya Hai na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro alisema wanafunzi watatumia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada ya vyuo.

“Mbio za nusu marathoni ziko pande mbili, upande mmoja zinashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao zawadi hizo za washindi zitawawezesha kulipia ada zao za vyuo, “alisema Kimaro.

Mtanzania atinga fainali Michezo Madola Bahamas

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania inayoshiriki Michezo ya Sita ya Vijana ya Jumuiya ya Madola, Regina Mpigachai.

Na Mwandishi Wetu
MWANARIADHA wa Tanzania Regina Mpigachai ametinga fainali ya mbio za meta 800 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa vijana inayoendelea Nassau, Bahamas.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Mpigachai alipangwa katika kundi la pili la mchujo na alimaliza mbio hizo akiwa katika nafasi ya tano kwa kutumia dakika 2:11.65.

Kundi la mchujo la mwanariadha huyo lilikuwa na wachezaji nane na alifuzu kucheza fainali baada ya kuwa mmoja kati ya wanariadha waliokuwa na muda mzuri zaidi licha ya kutokuwemo katika tatu bora.

Mshindi wa kwanza katika kundi la Mpigachai alikuwa Anna Lilly aliyetumia dakika 2.11.65 wakati mshindi pili ni Carlet Thomas.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema kuwa, Mpigachai kwanza ameboresha muda wake binafsi mpya baada ya ule wa awali wa dakika 2.13.51 aliouweka katika mashindano ya Kanda ya Tano yaliyofanyika Uwanja wa Taifa.

Bayi aliongeza kusema kuwa mwanariadha huyo pia pamoja na kumaliza watano, lakini muda wake ulikuwa bora zaidi akiwazidi wanariadha wote watatu wa kundi la mchujo wa kwanza waliotumia dakika 2.12.21, 2.12.84 na 2.12.86.

Wakati huohuo, mwanariadha mwingine wa Tanzania Francis Damian alitinga moja kwa moja katika fainali baada ya washiriki wa mbio hizo kuwa wachache.

Wanariadha wengine katika mbio hizo ni kutoka Kenya (mmoja), Canada (wawili), New Zealand (mmoja) na Scotland (mmoja).

Stars yatoka sare na Rwanda, yatupwa nje Chan

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas.

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imetolewa katika kinyang’anyiro cha kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kutoka suluhu na Rwanda katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amahoro nchini Rwanda.

Taifa Stars imeondolewa kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Rwanda katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na hivyo Stars ilikuwa ikihitaji angalau ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia bao 2-2.


Katika mchezo huo wa leo timu zote zilikosa mabao mengi baada ya kushindwa kutumia vizuri nafasi walizoata.

Kikosi cha Taifa Stars: 

1. Aishi Manula
2. Boniphace Maganga
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Salim Mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Raphael Daudi
11. Shiza Kichuya

Kikosi cha akiba

12. Said Mohamed
13. Hassan Kessy
14. Nurdin Chona
15. Salimin Hoza
16. Said Ndemla
17. Joseph Mahundi
18. Stamili Mbonde