Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Ujamaa Intellectuals Network (UIN) Jumapili ilitoa msaada
wa vifaa mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga kilichopo
Hananasif Kinondoni Moscow jijini Dar es Salaam.
Taasisi hiyo kupitia idara yake ya jamii, ilitoa vifaa hivyo
vilivyokabidhiwa kwa kiongozi na mmiliki wa kituo hicho Bi.Zainab Bakari Maunga
ni pamoja na unga, sabuni, madaftari, chumvi, juice, mafuta ya kula, mafuta ya
kupaka na vitu vingine.
Mratibu taifa wa UIN Lusekelo Mwandemange ndiye aiyekuwa wa kwanza
kukabidhi baadhi ya vifaa hiyo kwa Bi. Maunga kabla ya wana taasisi wengine nao
kukabidhi baadhi ya vifaa hivyo.
Kituo hicho kina jumla ya watoto yatima 49 huku baadhi yao wakiwa
ni wanafunzi wa chekechea, shule ya msingi na watatu wako sekondari.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Bi. Maunga alishukuru sana
kwa msaada huo na alitaka wasamaria wema wengine kujitokeza kuwasaidia kama
walivyofanya UIN.
Naye Mwandemange alisema mbali
na msaada huo, UIN pia kina mpango wa kuwasaidia wanafunzi hao watatu wanaosoma
sekondari.
Pia aliwataka watu na tasisi zingine kujitokeza kwa wingi kusaidia
kituo hicho ili kuhakikisha watoto hao yatima nao wanapata elimu kama watoto
wengine.
![]() |
Mkamiti Mgawe akibeba ndoo ya mafuta ya kula katika kituo cha watoto yatima |
No comments:
Post a Comment