Tuesday, 10 March 2015

McKinstry awania nafasi ya kuwa kocha wa RwandaKIGALI,Rwanda
RAIA wa Ireland ya Kaskazini Johnny McKinstry (pichani) yuko mbioni kuifundisha timu ya taifa ya Rwanda baada ya kuwamo katika orodha ya watu wanne wanaowania nafasi hiyo.

Wengine wanaowania kibarua hicho ni pamoja na kocha msaidizi wazamani wa Chelsea Jose Morais, kocha wa Uturiki Engin Fırat na Mjerumani Hans Michael Weiss.

Rwanda inaangalia mbadala wa kocha Muingereza Stephen Constantine, aliyejitoa tangu Januari na kwenda kuwa kocha wa timu ya taifa ya India.

Kocha wazamani wa Sierra Leone McKinstry,  29, inafikiriwa ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kunasa kibarua hicho.

Aliteuliwa kuwa kocha wa Leone Stars akiwa na umri wa miaka 27 na kuiongoza timu hiyo hadi kufikia nafasi ya 50 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), akipotezamchezo mmoja tukati ya sitaya kwanza.

Lakini kufuatia kufungwa na Ivory Coast na Kongo ya DRC katika fainali za Mataifa ya Afrika, alitimuliwa ikiwa ni miezi sita tu tangu alipopewa kazi hiyo kwa misingi ya kudumu.

Kocha Mreno Morais, 49, alifanya kazi kama msaidizi wa Jose Mourinho katika timu ya Inter Milan, Real Madrid na Chelsea kabla hajaenda timu ya Tunisia ya Esperance.

No comments:

Post a Comment