Thursday, 12 March 2015

Deni laifanya Fifa kuiondoa Zimbabwe Kombe la Dunia
HARARE, Zimbabwe
ZIMBABWE imeondolewa katika kinyanganyiro cha kufuzu kwa fainali za Kombe la dunia za mwaka 2018 baada ya nchi hiyo kushindwa kumlipa kocha wake wazamani Jose Claudinei Georgini.

Shirikisho la Kimataifa la Soka (fifa) limesema katika taarifa yake kuwa limechukua hatua hiyo kama matokeo ya kutolipa deni lake".

Fifa iliongeza kuwa Chama cha Soka cha Zimbabwe (zifa0 kilishindwa kufanya malipo licha ya kupewa muda kufanya hivyo.

Hatua hiyo ya kuifungia Zimbabwe kumemaliza nafasi ya nchi hiyo kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia mwaka 2018 hata kabla timu yao ya taifa haijagusa mpira.

Kanda ya Afrika inatarajia kuanza harakati za kusaka tiketi ya kucheza fainali hizo Oktoba, huku ratiba kamili inatarajia kupangwa huko St Petersburg mwezi julai, Zimbabwe haijawahi kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Mbrazil Georgini, aliyepewa jina la utani la Valinhos, na alianza kuifundisha timu hiyo januari hadi Novemba mwaka 2008. Na alikuwa akiidai Zifa na kwa mara ya kwanza Fifa ilikitaka chama hicho cha soka kumlipa kocha huyo mwaka 2012.

Zimbabwe mara kadhaa ilipewa hatmatamu na onyo lakini ilipuuza maagizo hayo ya Fifa. Fifa imesema kuwa Zimbabwe haikukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Zifa inakabiliwa na ukata mkali wa fedha, ikiwa na madeni karibu dola za Marekani Milioni 4, na hivi karibuni iliuzaa vifaa vyake vilivyomo katika kituo cha mazoezi ilichojengewa na Fifa ili kupunguza ukata huo.

No comments:

Post a Comment