Tuesday, 10 March 2015

Porto nayo yatinga robo fainali mabingwa UlayaPORTO,Ureno
KLABU ya Porto kwa mara ya kwanza imefuzu kucheza hatua ya nane bora (robo fainali) ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya tangu mwaka 2009 baada ya kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Basel.

Kikosi hicho cha Wareno hakikuwa na mfungaji wake wa mabao mengi Jackson Martinez, lakini walifanikiwa kuzifumania nyavu mara nne wakati Yacine Brahimi akifunga kwa bao la mpira wa adhabu la umbali wa mita 20.

Hector Herrera aliongeza ushindi wa timu yake kabla Casemiro hajafunga tena kwa mpira wa adhabu.

Baadae Vincent Aboubakar aliongeza la nne kabla Walter Samuel hajapata kadi nyekundu wakati Porto ikiongeza rekodi yake ya kutofungwa katika mashindano haya hadikufikia mechi 10.

Porto ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2004 walipata misukosuko kidogo kutoka kwa timu hiyo ya Uswisi, ambayo ilifuzu kutoka katika hatua ya makundi badala ya Liverpool.
 Na ingawa timu nyingi za Ulaya zitaona kama Porto ni timu nzuri ya kukutana nayo katika robo fainali, timu hiyo imeimarika zaidi ikiwa chini ya kocha Muhispania Julen Lopetegui.

No comments:

Post a Comment