Friday 6 March 2015

Mwanariadha aliyejilipua Glasgow asota London



 *Hana uhakika wa chakula na kulala kwake ni bustanini

Jimmy Thoronka.
LONDON, England
MKIMBIAJI wa mbio fupi kutoka Sierra Leone aliyeingia mitini baada ya kumalizika kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola huko Glasgow, amekuwa akiishia kwa kutangatanga jijini hapa.

Jimmy Thoronka, 20, ambaye ni miongoni mwa wakimbiaji 100 bora nchini mwake lakini hakurejea nchini huko mwaka jana akidai kuwa alikuwa akihofia ugonjwa hatari wa Ebola.

Thoronka asiye na makazi anasema kuwa Ebola imeua ndugu zake wa karibu huko Sierra Leone.

"Wakati mwingine sipaji kabisa chakula. Naosha vyoo vya jumuiya na kulala katika bustani," aliliambia the Guardian.

Thoronka aliwasili Glasgow na wachezaji wenzake Julai 2014 wakati ugonjwa wa Ebola ukiwaumefumuka nchini kwao huku nchi hiyo ikitangazwa kuwa sehemu ya karantini ya ugonjwa huo.

Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo nchini Sierra Leone hadi sasa ni zaidi ya 3,500.

Hadi wachezaji 30 wa nchi hiyo walitaka kuongeza viza yao kutoka Septemba mwaka jana ili waweze kuendelea kukaa Uingereza.

Thoronka, alielezewa na Chama cha Riadha cha Sierra Leone kama "mkimbiaji wa aina yake, mwenye uwezo na kasi ya ajabu ", aliyeshindana katika mbio za kupokezana vijiti ya mita 4x100 katika michezo hiyo, lakini alishindwa kutwaa medali yoyote.

Aliweka muda wake bora wa sekunde 10.58 katika mbio za mita 100 kabla ya mashindano hayo.

Katika mahojiano, Thoronka alidai kuwa: Aliambiwa wakati wa michezo hiyo kuwa mjomba wake aliufa "huenda kutokana na Ebola " na "hakuweza kumnyamazisha kulia."

Hati yake ya kusafiria iliibwa Glasgow hivyo anaishi na rafiki yake huko Leicester.

Thoronka alishinda medali katika mashindano ya Afrika na alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa Sierra Leone wa mwaka 2013 inayotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo.

Ndiye alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Sierra Leone kubeba Kifimbo cha Malkia na kikimbia nacho katika Michezo ya Jumuiya ya Madola.

No comments:

Post a Comment