Thursday, 5 March 2015

Evans, Cisse kufungiwa kwa kutemeana matePicha tofauti zikiwaonesha  Jonny Evans na Papiss Cisse wakitemeana mate kwenye uwanja wa St James' Park.
LONDON, England
BEKI wa Manchester United Jonny Evans na mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse huenda wakakabiliwa na kifungo hadi cha miezi sita endapo watapatikana na hatia ya kutemeana mate.

Wawili hao walinekana wakitemeana mate wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumatano usiku kwenye uwanja wa St James' Park.

Mwamuzi wa mchezo huo Anthony Taylor alizungumza na Evans na Cisse baada ya tukio hilo la kipindi cha kwanza, lakini hakuna aliyepewa kadi.

Hatahivyo, Chama cha Soka cha England kinasema kuwa kinasubiri taarifa ya mwamuzi kabla ya kuamua kama watachukua hatua yoyote.

Msimu uliopita, George Boyd alifungiwa mechi tatu kwa kumtemea mate kipa wa Manchester City Joe Hart.
Wachezaji kadhaa wazamani wanaamini kuwa Evans na Cisse wanastahili adhabu.

Kiungo wazamani wa Newcastle Dietmar Hamann alielezea kuwa kitendo hicho "kamwe hakikubaliki".

Picha za televisheni zilimuonesha Evans akimtemea mate Cisse, aliyekuwa chini.

Naye mshmabuliaji huyo wa Senegal alionekana kutema mate upande wa Evans.

Sio kocha wa Newcastle John Carver au mwenzake wa Manchester United Louis van Gaal aliyesema kama aliona kitendo hicho.

"Siwezi kusema lolote kuhusu hilo, " alisema Carver, ambaye timu yake ilifungwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment