![]() |
Gerard Pique wa Barcelona (kulia) akimiliki mpira katika moja ya mechi za La Liga. |
MADRID, Hispania
BEKI wa Barcelona Gerard Pique anasema kila upande una
nafasi sawa ya kushinda pambano la Jumapili la Clasico dhidi ya wapinzani
wadogo Real Madrid.
Klabu hiyo ya Catalan iko pointi moja mbele ya Real
Madrid kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga.
"Kila upande una nafasi ya asilimia 50 ya
kushinda. Wana Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, wachezaji wawili wenye nguvu
sana, kasi kubwa, hatari sana na wanafunga mabao."
Real Madrid ilishinda mechi mbili za mwisho za Clasicos,
na inaweza kuwa mara tatu mfululizo kwa mara ya tatu tangu mwaka 1978.
Hatahivyo, Barcelona haijawahi kupoteza mchezo kwenye
uwanja wake wa nyumbani tangu ilipoingi katika ligi mwaka 1929-30.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alifunga mabao
17 katika La Liga mwaka 2015, ikiwa ni zaidi ya wachezaji watatu wa Real Madrid
Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo combined. Wamefunga mabao
matano tu kila mmoja.
Pique aliendelea: "Huu ni moja kati ya mchezo
maalum wa mwaka, kwa sababu upinzani kati yetu na tunacheza kama kawaida dhidi
yao.
Timu nyingine kubwa, yenye wachezaji wakubwa na hilo
ndilo linafanya kuwa maalum zaidi."
Barca imeshinda mara tisa kati ya mechi 10 za mwisho za
La Liga na Pique alisema: "Unajihisi una nguvu zaidi na kujiamini….
"Kushinda mechi ya Clasico kutakuwa ni kupiga hatua kubwa mbele. Kuna mechi 10 zimebaki na tumekaribiana sana."
Mshambuliaji wa Real Madrid Benzema alisema: "Tunajua
mchezo utakuwa na presha kubwa, lakini hilo ni kawaida kwa kuwa ni mechi kubwa.
"Kila mchezaji anayependa soka anataka kucheza
mchezo huo. Endapo tutazuia vizuri tutapata matokeo mazuri.
"Tunaweza kurudia matokeo ya kushinda 3-1 katika
mchezo wa kwanza. Tuko katika hali nzuri kushinda na kucheza vizuri kama
tulivyocheza awali.
"Kufunga tena kama tulivyofanya katika mchezo ule
wa kwanza wa msimu, kiasi fulani kunahitaji bahati na wala hakuna jambo jingine."
No comments:
Post a Comment