Monday, 30 May 2016

Tamasha la tisa la michezo la shule za filbert Bayi lafana kwa kuibua vipaji kibaoMwandishi Wetu, Kibaha
TAMASHA la tisa la michezo la shule za Filbert Bayi lilikamilika juzi huku vipaji kibao vikiibuka katika michezo mbalimbali.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shule hizo Filbert Bayi, tamasha hilo hufanyika kila mwaka na lengo likiwa kuibua vipaji vya michezo kwa wanafunzi wa shule hizo za msingi na sekondari zilizopo Kimara na Kibaha, Mkuza.
alisema wanafunzi mbali na kutia bidii katika masomo, pia wanatakiwa kucheza ili kuibua vipaji vyao na kujijenga kiafya na kiakili.

Michezo ya Riadha, soka, kuvuta kamba, kuruka chini, kukimbia na magunia, kukamata kuku, kukimbia na kupasua maputo ilishindaniwa katika bonanza hilo la kusisimua, ambalo pia timu ya waandishi wa habari ya Habari Sports ilialikwa.

Warekodi muda wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa mbio za meta 1500.
Katika mchezo wa soka, timu ya Habari Sports (iliyoalikwa) ilitoka sare ya kufungana mabao 5-5 na timu ya shule ya Filbert Bayi katika mchezo uliofanyika Mkuza, Kibaha.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Filbert Bayi walikuwa mbele kwa mabao 3-1 na kuwafanya Habari Sports kuwa na kibarua cha kurudisha mabao.

Watoto wakichuana katika mbio za meta 50.
Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya Kimara iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenzao wa Kibaha katika mchezo uliofanyika kwenda uwanja wa Soka wa shule hizo Mkuza.

Bao hilo pekee liliwekwa kimiani na Juma Gwila na kuiwezesha timu yao kutwaa ubingwa wa soka kwa wanafunzi wakiume.

Mkurugenzi Msaidizi wa shule za Filbert Bayi, Elizaberth Mjema akishuhudia mbio hizo.
Tamasha hilo ni la kila mwaka na limekuwa likiibua vipaji kwa ajili ya kuviendeleza na tayari kuna wanariadha wanaosoma katika shule hizo na wapo katika timu ya taifa ya mchezo huo.

Mwenyekiti wa shule hizo, Filbert Bayi alisema kuwa tamasha hilo linalengo la kuibua vipaji na sasa wanajiandaa kwa kuandaa wachezaji kwa ajili ya Michezo ya 32 ya Olimpiki yatakayofanyika Japan 2020.

Viongozi wa shule za Filbert Bayi, Mr Kagonso (kulia), Filbert Bayi, Anna Bayi, Elizaberth Mkema na Arrieth.
Bayi ni bingwa wazamani wa dunia wa mbio za mita 1500 na zile za maili moja huku hadi leo akishikilia rekodi ya Jumuiya ya Madola ya mbio za mita 1500 aliyoiweka mwaka 1974 Christchurch, New Zealand.
DJ `mtoto' wakati wa tamasha la tisa la michezo la shule za Filbert Bayi Kbaha mwishoni mwa wiki.
Ufunguzi wa tamasha hilo ulianza kwa maandamanao.
   
Wanafunzi akiapa kwa niaba ya wachezaji.
Mwalimu akiapa kwaniaba ya waamuzi wa michezo ya tamasha hilo.
 
 
 
 

Habari Sports Club wakichuana katika mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya wafanyakazi wa Filbert Bayi. Habari walishinda kwa upande wa wanaume.

Filbert Bayi wakivutana na Habari Sports (hawapo pichani)
Habari Sports Club wakivutwa na Filbert Bayi (hawapo pichani).
Filbert Bayi wakicheza baada ya kuwabwaga Habari Sports katika kuvuta kamba.

Wanariadha wa Habari Sports wakimaliza mbio za meta 100.

 
Timu ya netiboli ya Filbert Bayi ikipozi.
Mchezaji wa timu ya taifa ya riadha, mbaye ni mwanafunzi wa shule ya Filbet Bayi, Rose Seif akiruka chini katika tamasha hilo.


Thursday, 26 May 2016

RT, Azania Bank watangaza zawadi za Kids Run zitakazofanyika Mei 5 kwenye viwanja vya mnazi mmoja kutumia Sh. Milioni 130 na ushee


Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Azani, Othman Jibrea(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT). Kulia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RT, Tullo Chambo.

Na Mwandishi Wetu
RIADHA Tanzania (RT) kwa kushirikiana na Benki ya Azani, leo wametangaza zawadi kwa washindi wa mbio za watoto, Kids Run, zitakazofanyika Juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RT, Tullo Chambo alisema  mbio hizo zitakuwa katika vipengele vitano vya umbali wa kilometa tano, mbili na moja, huku zingine ni meta 100 na meta 50 kwa wavulana na wasichana kulingana na umri.
 
Alisema wale wa kilometa tano, mbili na moja wenyewe watapita katika barabara mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kumalizia mbio hizo katika viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja walikoanzia.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Kids Run zitakazofanyika Mei 5 jijini Dar es Salaam.
Alisema maandalizi yanaenda vizuri na ni matarajio yao kuwa zaidi ya watoto 2,000 watajitokeza kushiriki katika mbio hizo za kwanza na aina yake kushirikisha watoto.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Azani, Othman Jibrea alisema kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa tano ataondoka na sh. 200,000, suti ya michezo na vifaa vya shule.

Mratibu wa Kids Run, Wilhelm Gidabuday akizungumza leo kuhusu mbio hizo. Kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Azania, Othman Jibrea.
Mshindi wa pili atapewa sh. 150,000 suti ya michezo na vifaa vya elimu, wakati mshindi watatu atapewa sh. 100,000 na vifaa vya elimu.

Mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa mbili ataondoka n ash. 100,000, wakati wa pili atapewa sh. 75,000 na watatu sh. 50,000, ambapo wote mbali na zawadi za fedha watapewa vifaa vya shule.
 
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania, RT, Tullo Chambo.
Jibrea alisema washindi wa kilometa moja watapata zawadi za sh. 75,000, 50,000 na 40,000 pamoja na vifaa vya shule.
Alisema kuwa washindi wote pia watafungiliwa akaunti katika benki ya Azani, ambako watawekewa zawadi zao hizo.

Aidha, Benki ya Azani imesema kuwa itatumia zaidi ya Sh.Milioni 130 kugharamia mashindano hayo, ambayo ni ya kwanza na ya aina yake kufanyika hapa nchini.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Azani, Othman Jibrea akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Kids Run.
 Watoto wa umri tofauti wanatarajia kuchuana vikali katika mbio hizo za Kids Run Mei 5, 2016.