Monday 26 January 2015

Didier Drogba anyakua tuzo ya waandishi

MSHAMBULIAJI Nyota wa Chelsea, Didier Drogba amepewa tuzo ya mchango wake katika soka.
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo, FWA kimempa tuzo hiyo Drogba ambaye aliwahi kuitwaa David Beckham na Alex Ferguson.
Drogba amesisitiza aniifurahia tuzo hiyo lakini akasema angependa kubaki Chelsea hata baada ya kustaafu.

Miss Colombia ndiye Miss Universe 2015

Miss Colombia, Paulina Vega baada ya kuvishwa taji la Miss Universe 2015.
Miss Jamaica Kaci Fennell (22) aliyetarajiwa na wengi kutwaa taji hilo.
Kaci Fennell aliwataja Bob Marley na Usain Bolt kuwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa dunia kutoka nchini mwake.
Miss Universe 2015, Paulina Vega akiwa katika vazi la taifa lake.
 Mashabiki wa Miss Jamaica baada ya matokeo hayo walivamia mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter kumtangaza mrembo huyo aliyejipatia umaarufu pengine zaidi ya mshindi.
 Mashabiki wa Miss Jamaica baada ya matokeo hayo walivamia mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter kumtangaza mrembo huyo aliyejipatia umaarufu pengine zaidi ya mshindi.
MISS Colombia, Paulina Vega atwaa taji la Miss Universe 2015 katika fainali zilizofanyika jana huko Miami nchini Marekani huku umati ukizomea kuonyesha kutoridhika na matokeo hayo.
Umati uliohudhuria fainali hizo ulitarajia Miss Jamaica Kaci Fennell aliyeshika nafasi ya nne kutwaa taji hilo lakini ulionyesha kushangazwa na maamuzi ya majaji kumtangaza Miss Colombia Paulina Vega mwenye miaka 22.
Zomea zomea zilisikika mara baada ya mshindi huyo kutangazwa huku kukiwa na minong'ono ya hujuma katika mashindani ya mwaka huu.