Sunday, 15 March 2015

Angel Di Maria kuendelea kuwepo Man United msimu ujaoAngel Di Maria (kushoto) akiwa na kocha wake.tion

LONDON,England
WINGA Angel Di Maria amehakikishiwa kuwemo katika orodha ya wachezaji wa klabu ya Manchester United msimu ujao, kwa mujibu wa kocha Louis van Gaal.

Mchezaji huyo ambaye yuko katika kiwango kibovu na alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Kombe la FA war obo fainali wakati timu yake ilipofungwa 2-1 na Arsenal kulikuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa kitita ch rekodi cha pauni Milioni 9.7, alikuwa akisaka timu kuondoka.

Lakini Van Gaal alisema: "nafikiri ataendelea kuwemo katika timu hii.  Tabia yake na ari yake baada ya ile kadi nyekundu ni nzuri tu."
Mholanzi huyo alisema pia kuwa wamiliki wa klabu hiyo ambao ni familia ya Glazer, wameridhishwa na kazi yake ya ukocha.

Hatahivyo, baadhi ya vyombo vya habari mjini hapa vilisema kuwa kocha huyo yuko tayari kumuachia mchezaji huyo kuondoka katika timu hiyo kwa sababu zake za kibinafsi lakini kibiashara hailipi.

No comments:

Post a Comment