Thursday, 12 March 2015

Rais Real Madrid akanusha kutimuliwa kwa kocha Ancelotti
MADRID, Hispania
RAIS wa Real Madrid Florentino Perez ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuelezea kumuunga mkono kocha Carlo Ancelotti na kumtetea Gareth Bale aliyekalia kuti kavu katika timu hiyo.

Marca, gazeti maarufu la michezo la jijini hapa, lilidai kuwa, kocha huyo wazamani wa Chelsea alikaribia kutupiwa virago, ulisomeka ukurasa wake wa mbele, huku ukiwa na kichwa cha habari: 'Hakuna Zaidi'.

Marca ilidai kuwa kipigo cha timu hiyo dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp ndani ya siku 10 kutashuhudia mwisho wa Ancelotti, aliyeiongoza timu hiyo kutwaa mataji mawili lile la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na la Mfalme.

Lakini, akionekana kujibu moja kwa moja ripoti ya gazeti hilo, Perez alisema: 'Taarifa hizo sio za kweli na hazikubaliki kabisa kwa sasa

Napenda kutoa maelezo kwa mpangilio kuwa klabu ina imani kubwa na kocha wetu na wachezaji pia. Na ninataka kusema kuwa, nina kanusha vikali taarifa hizo na siku zijazo na wiki Carlo Ancelotti atabaki kuwa kocha wa Real Madrid. 

'Mimi kama rais wa Real Madrid, nawaomba mashabiki wetu kumuunga mkono kocha na wachezaji wetu na ninawaomba kujisikia fahari kuwa nao.'

Real haijashinda katika michezo yake mitatu, na kuachia uongozi ea Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga kwa Barcelona na imefuzu kibahati kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa faida ya bao la ugenini baada ya kuchapwa 4-3 nyumbani na Schalke Jumanne usiku.

No comments:

Post a Comment