![]() | |
Baadhi ya wachezaji wa timu ya netiboli ya Uhamiaji wakati timu za tanzania zilipoagwa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Zanzibar. |
Na Seba Nyanga
TIMU za netiboli
za JKT Mbweni, Uhamiaji Tanzania na JKT Ruvu zimeagwa leo na mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Timu hizo ambazo
zilikabidhiwa bendera na Malinzi zitashiriki mashindano ya Afrika Mashariki
yatakayofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Jumamosi Machi 14.
Malinzi
aliwakabidhi bendera ya taifa manahodha wa timu hizo, Zakia Kondo wa Uhamiaji,
Panina Mayunga wa JKT Mbweni na Anitha Elius wa JKT Ruvu.
Mwenyekiti huyo wa
BMT ambaye hii karibuni aliteuliwa tena kushika wadhifa huo kwa kipindi kingine
cha miaka mitatu baada ya kumaliza kile cha mwanzo aliwataka wachezaji hao
kwenda Zanzibar kushindana na si kushiriki.
Malinzi alisema
kuwa ana usongo na mataji kwani katika kipindi chote cha uongozi wake ndani ya
BMT hajawahi kuona medali, hivyo huu ni wakati wake wa kushuhudia ushindi.
Naye mwenyekiti wa
Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) Annie Kibira aliwataka wachezaji wa timu
hizo kuwa na umoja na kuacha maneno maneno.
“Mtakakuwa
Zanzibar mjitahidi sana kuwa wamoja kama wenzenu Wanzanzibar wanavyokuja huku
na msiwe na idomo domo, “alisema Kibira
katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa BMT Henry Lihaya.
![]() |
Baadhi ya iongozi na wachezaji wa timu za Uhamiaji, JKT Mbweni na JKT Ruvu wakimskiliza mwenyekiti wa BMT (hayopo pichani0 wakati wakuziaga timu hizo. |
![]() | |||||||||||||||
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Uhamiaji na JKT Mbweni wakichuana katika mchezo wa kirafiki jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Uhamiaji | walishinda |
No comments:
Post a Comment